STAA wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie amesema kuwa amepitia wakati mgumu kipindi alichotangaza kudai talaka kwa mume wake, Brad Pitt ambaye pia ni mcheza filamu.
Jolie amesema kuwa hakufurahishwa na uamuzi wake kwa sababu ulianza kumsababishia tatizo la kukosa usingizi nyakati za usiku akiwaza hatma ya uamuzi wake.
“Nimepitia wakati mgumu sana kwasababu sikufurahia hali ya kutokuwa na mpenzi, si jambo nililolitaka, hakuna kitu chochote kizuri kuhusiana na hilo. Ni jambo gumu sana,” alisema staa huyo.