BINGWA wa ndondi katika uzani mzito duniani, Tyson Fury amesema amekuwa akitumia cocaine ili kumsaidia kukabiliana na matatizo ya kiakili.
Bondia huyo wa Uingereza amesema kuwa amekuwa akiugua ugonjwa wa akili kwa miaka kadhaa na hajafanya mazoezi tangu mwezi Mei.
“Nimekuwa nje nikilewa, Jumatatu hadi Ijumaa na Jumapili na kutumia cocaine,” Fury aliliambia jarida la Rolling Stones.
Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya Fury kudai katika mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu, kabla ya kukutana na madai hayo saa tatu baadae akisema alikuwa akifanya utani.
Akizungumzia kuhusu masuala ya afya yake, Fury aliongezea: “Siwezi kukabiliana na matatizo hayo na kitu kinachonisaidia ni wakati ninapokunywa ili nitoe matatizo hayo akilini.
Wanasema nina ugonjwa wa akili. Nahisi huzuni na ningependa mtu aniue kabla sijajiua.”