Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

LUCAS VAZQUEZ WA REAL MADRID ALIVYODHIHIRISHA KUWA ANA MAPAFU YA MBWA

$
0
0

LUCAS VAZQUEZ ameonyesha kuwa “ana mapafu ya mbwa” kuliko wachezaji wenzake wote wa Real Madrid baada ya kukimbia umbali mrefu zaidi katika mechi ya nusu fainali ya Champions League Uwanja Etihad, dhidi ya Manchester City, Jumanne usiku.

Mhispania huyo alikimbia kilomita 13.3, huku nyota mwenzake aliyemkaribia akiwa Toni Kroos aliyekimbia kilomita 11. Kevin De Bruyne na Fernandinho walikuwa vinara wa mbio kwa Manchester City wakikimbia kilomita 11.5 kila mmoja.

Vazquez alipata nafasi ya kuanza mechi hiyo kuziba nafasi ya Cristiano Ronaldo aliyebaki benchi kwa kuwa majeruhi, na akamshukuru kocha wake Zinedine Zidane kwa kumpa fursa mbele ya mastaa wengine wazoefu kama James Rodriguez, Isco na Jese Rodriguez.

Rekodi za winga huyo wa zamani wa Espanyol, zinampa sifa ya “kujituma kama farasi” akiwa na jezi ya Real Madrid, akiwa mchezaji pekee wa timu hiyo aliyeandika rekodi ya kukimbia umbali mrefu kuliko wote katika Champions League msimu huu.

Katika mechi dhidi ya AS Roma walipokutana raundi ya timu 16, Vazquez alikimbia kilomita 12.08 Estadio Santiago Bernabeu, na katika hatua ya makundi dhidi ya Paris Saint-Germain alimudu kukimbia kilomita 12.07.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>