
KIUNGO nyota wa Arsenal aliyeandika rekodi ya kutengeneza nafasi 137 katika Premier League msimu huu, Mesut Ozil, amesema hana haraka ya kusaini mkataba mpya na anaweza kusubiri hadi mwisho wa msimu kwa mazungumzo na klabu hiyo.
Ozil aliyepika mabao 18 msimu huu, kama ilivyo kwa mwenzake Alexis Sanchez wamebakisha miaka miwili katika mikataba yao ya sasa, huku Arsenal ikidhamiria “kuwatia pingu” kwa kuwapa mikataba mirefu zaidi kiangazi hiki.
Akizungumza katika mahojiano na Sport-Informations-Dienst ya Ujerumani, Ozil aliyeandikaalisema: "Hakuna haraka. Nina miaka miwili imebaki katika mkataba wangu. Tutaona itakavyokuwa mwisho wa msimu."