
Manchester United inakaribia kukamilisha dili la usajili wa pauni milioni 46 kwa kiungo kinda wa Benfica Renato Sanches.
United ilikuwa kwenye maongezi ya kina tangu mwezi Januari kwaajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 na Alhamisi usiku rais wa Benfica Luis Filipe Vieira alitua London kwaajili ya kukamilisha maongezi ya dili hilo.
Sanches yupo Benfica kwa mkataba wa hadi mwaka 2021 na ana kipengele kinachomruhusu kuondoka kwa pauni milioni 60, lakini inaaminika klabu hiyo iko tayari kupokea pauni milioni 31 mwanzoni mwa dili na milioni 15 baadae.
Kiungo huyo ameichezea Benfica mechi 22 msimu huu na kufunga magoli mawili huku akiitwa timu ya taifa na kuichezea mechi mbili.
Inaaminika Sanches ndiyo kipaji kipya cha kipekee Ureno kinchokuja baada ya Cristiano Ronaldo.
Sanchez na yeye pia anawakilishwa na wakala wa Ronaldo - Jorge Mendes.

Sanchez ananukia United kwa pauni milioni 46

Manchester United ilimsajili kinda wa Ureno enzi hizo Cristiano Ronaldo (kulia) mwaka 2003