Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Article 4

$
0
0
KOCHA wa zamani wa Mashetani Wekundu, Alex Ferguson amemwambia Louis Van Gaal kuwa kama atabahatika kuendelea na kibarua cha kubakia Old Trafford aache kabisa kjusajili wachezaji maarufu.

Kisha akampa sababu na kusema, baadhi ya wachezaji maarufu na wenye majina makunbwa hubweteka pindi wanaposajiliwa, hivyo huwa hawana msaada katika timu.

Ferguson aliyasema hayo baada ya kushuhudia United imeanza kukata tama ya ubingwa na sasa inasaka nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu wa mwakani.

“Nina jambo la kumshauri Van Gaal. Kama atabahatika kubakia kama kocha wa United basi aige mfano wangu wa kutosajili wachezaji wengi wenye majina makubwa na maarufu.”

“Kusajili wachezaji wengi nyota ni sawa na kujiangusha mwenyewe kwani baadhi yao hubweteka pindi wanaposajiliwa na klabu kubwa mfano wa Manchester United, badala yake aangalie wachezaji walio na vipaji lakini wa umri mdogo.”

“Mimi nilifanya hivyo kwa wachezaji wengi akiwemo Ryan Gigs, Rio Ferdinand, Christiano Ronaldo na hata Wayne Rooney. Ingawa walikuwa hawana majina, lakini walikuja kuwa hadhi ya timu.”

“Kisha lazima kocha kama wa united aangalie utamaduni wa soka la England ambalo ni la kujali zaidi wachezaji wanaoweza kudumu kikosini kwa kipindi kirefu,” alisisitiza Ferguson.

Kaulki ya Ferguson ni kama inaungana na ile ya Arsene Wenger ambaye aliwahi kumweleza Van Gaal kuwa lazima awe na uzoefu wa Ligi ya England na aina ya wachezaji anaowasajili, lakini pia Wenger alimtaka van Gaal kuacha kufanya usajili wa mara kwa mara kwani unaifanya timu kuwa mpya kila siku, hatua ambayo si njema kwani timu hushindwa kujijenga.

   

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>