Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

DUDUBAYA AJIRUDI KUTAKA CHID BEENZ AFE... sasa amwombea dua apate afya njema arejee kwenye gemu kwa kasi

$
0
0
VETERANI wa  muziki wa Kizazi Kipya, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amemuombea afya njema Chid Beenz na kumtaka apone haraka kwa madai kwamba Bongofleva bado inamuhitaji.

Dudubaya amemtakia afya njema msanii mwenzake huyo ikiwa ni wiki chache tangu aseme kuwa watu wanaotumia dawa za kulevya kama Chid Beenz wanatakiwa kuachwa wafe.

“Ingawa kuna watu walionilaumu kwa kauli hiyo wakitaka niombe radhi, siwezi kufanya hivyo, ninachoweza ni kumpa pole kwa matatizo yaliyompata na ninaomba Mungu apate nguvu mpya, akili mpya na mwanga mpya kwani Bongofleva bado inamuhitaji,” alisema Dudubaya.


Chid kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kukubali kupelekwa Bagamoyo mkoani Pwani, kwenye kituo maalum cha tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles