Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

BARCELONA WAPIGA HESABU ZA KUMUUZA NEYMAR

$
0
0
MABINGWA wa Hispania, Barcelona wanafikiria uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wake Neymar (24), ambapo sababu kubwa wameieleza kuwa hawawezi kuingia nae mkataba wa muda mrefu.

Klabu hiyo imechanganyikiwa juu ya uwezekano wa kuendelea kuwa na mshambuliaji huyo wa kimataifa Brazil, ambaye mkataba wake unamuingizia pauni mil. 144.

Aidha, sababu nyingine inayoifanya klabu hiyo kutaka kumuuza mshambuliaji huyo ni hatua ya kutaka kuongezewa mshahara wake wa sasa wa pauni 77,000 kwa wiki.

Huku Barcelona ikionekana kumchoka mshambuliaji huyo, Manchester United iko kinywa wazi ikitaka kumsajili ambapo imemuahidi kumlipa pauni mil. 300,000, huku pia klabu ya PSG nayo ikimtaka mshambuliaji huyo.

Aidha, klabu hiyo imeeleza kuwa sasa inakabiliwa na tatizo la kifedha, hasa ikikumbukwa kuwa haina mdhamini wa uhakika wa jezi ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Sky Sports nchini Hispania, Guillem Balague, klabu hiyo ipo kwenye wakati mgumu juu ya sakata la Neymar.


“Bila ya kuwa na mdhamini wa uhakika sifikirii klabu ya Barcelona inaweza kuwaongezea mkataba Neymar, Messi na Luis Suarez,” alisema Balague.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>