Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

PICHA 8: MAMBO YAZIDI KUNOGA, MAKONDA AKUTANA TENA NA WADAU WA MUZIKI MCHANA HUU

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amekutana na Kamati ya muda ya wadau wa muziki na wamiliki wa bar na kumbi za starehe mchana huu ikiwa ni mwendelezo wa maagizo aliyotoa jana mchana katika mkutano wa wadau wa muziki uliofanyika Vijana Social Hall Kinondoni.

Mheshimiwa Makonda amekutana na wajumbe wa kamati hiyo ofisini kwake Ilala Dar es Salaam.

Katika mkutano wa Alhamisi, Makonda aliwataka wamiliki wa bar, kumbi za starehe, viongozi wa bendi na wanamuziki kutii sheria ya kumaliza muda wa maonyesho yao hadi pale sheria hiyo itakapobadilishwa.

Aidha mkuu huyo wa mkoa aliitaka kamati ya muda ya wanamuziki na wamiliki wa bar na kumbi za starehe iandae mapendekezo ya kubadili sheria hiyo, mapendekezo ambayo yatakuwa na hoja zenye mashiko na ushawishi waå kutosha uliojaa hoja za msingi.

Katika kutekeleza agizo la mkoa, ndipo kamati hiyo ilipowasilisha mapendekezo yao leo hii mbele ya Mkuu wa Mkoa na bila kusita akaanza kuifanyia kazi papo hapo.

Moja ya ombi kubwa la kamati hiyo ni ile inayohusu kurefushwa kwa muda wa maonyesho ya muziki kutoka saa 6 usiku hadi saa 8 za usiku.

Makonda akamuhusisha pia Mshauri wa Biashara wa Mkoa ili kupitia sheria ya kumaliza shughuli za muziki saa 6 za usiku.

Baada ya kujadiliana kwa muda, Mkuu wa Mkoa aliahirisha kikao hicho kwa muda masaa machache na kuagiza maafisa utamaduni na maafisa biashara wa wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala wawepo katika awamu ya pili ya mkutano huo utakaofanyika baadae mchana huu.

Wajumbe wa kamati hiyo ya wadau wa muziki na wamiliki wa bar na kumbi za starehe waliokwenda kuonana na Mkuu wa Mkoa ni pamoja na Juma Mbizo, Siza Mazongela, Juma Jerry “JJ”, Mponjoli Mwakabana na Said Mdoe.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akifanya mkutano na kamati ya muda ya wadau wa muziki na wamiliki wa bar na kumbi za starehe leo mchana
 Kulia ni Mashauri wa Biashara wa Mkoa wa Dar es Salaam akitoa mapendekezo kadhaa
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akisikiliza hoja kwa makini
 Kushoto ni mwenyekiti wa muda wa kamati bwana Juma Mbizo
 Kushoto ni katibu wa muda wa kamati Siza Mazongela na kulia ni mjumbe wa kamati Mponjoli Mwakabana
 Waandishi wa habari wa Channel Ten na walikuwepo 
Umati unaoonekana kwa mbele ni sehemu ya wananchi wanaosubiri kumuona mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa shida zao mbali mbali


Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>