Baada ya kusukwa upya bendi ya Double M Sound inayoongozwa Mwinjuma Muumin, sasa itajulikana kama Double M Plus.
Mwinjuma Muumin amesema ameamua kukarabati jina la bendi yake ili kwenda sambamba na mabadiliko makubwa aliyoyafanya.
Muumin amedai Double M Plus itaibuka na nyimbo mpya zitakazoendana soko la sasa hivi ikiwa na wasanii wapya wenye uwezo wa hali ya juu.
Bendi hiyo imetambulisha wanamuziki wake wapya wakiwemo Dogo Rama, Saleh Kupaza na Jojoo Jumanne kutoka Twanga Pepeta.
Naye Saleh Kupaza amesema anashuka na wimbo mpya Double M Plus ambao utajulikana kama “Ganda la Mua”.
“Hii sio ile niliyotunga Twanga Pepeta, kwanza Twanga walilikataa lile jina, ninachojua mimi ni kwamba wimbo wangu ule hauna jina na umeachwa ukipotea kwa makusudi, kwahiyo “Ganda la Mua” inakuja kivingine ndani ya Double M Plus,” alisema Kupaza katika maongezi yake na Saluti5.