Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live

CHELSEA BADO HAIJAMKATIA TAMAA JOSE MOURINHO

$
0
0
Jose Mourinho has endured a torrid season as Chelsea boss with the champions sitting 16th in the table
UONGOZI wa klabu ya soka ya Chelsea umeanza kazi ya kutafakari jinsi gani utafanya ili timu hiyo iweze kufanya vizuri.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari nchini Uingereza, imeeleza kuwa viongozi wa klabu hiyo wanajipanga upya.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuvuja habari kwamba huenda kocha Jose Mourinho atatimuliwa wakati wowote.

Tayari habari zaidi zimeeleza kuwa huenda klabu hiyo ikamchukua kocha mmojawapo kati ya Brendan Rodgers, Roberto Di Matteo na Guus Hiddink.
Hata hivyo Chelsea imesema bado ina imani na Mourinho na kwamba inajipanga upya kupitia yeye huku ikiamini kuwa kocha huyo bado ana uwezo wa kuirejesha klabu kwenye enzi za ushindi.
Chelsea inatarajiwa kufanya marekebisho kadhaa katika kikosi chake kwenye usajili wa dirisha dogo kabla ya kukifumua upya pale utakapowadia muda wa usajili wa majira ya kiangazi baada ya msimu huu kumalizika.

NEW AUDIO: SIKILIZA NA UJIPAKULIE WIMBO MPYA “PENDO LA UKAKASI” WA SAIDA RAMADHAN AKIWA NA MASHAUZI CLASSIC

$
0
0


Hii ni moja ngoma mpya kali za Mashauzi Classic Modern Taarab chini yake Isha Mashauzi.

Wimbo unaitwa “Pendo la Ukakasi” ukiwa umeimbwa na Saida Ramadhan ukipenda Saida Mashauzi ambapo umeachiwa rasmi Novemba 14, 2015.

Ni utunzi wake Isha Ramadhan. Gitaa la solo limecharazwa na Mfaume, bass kasimama J Four Boya wakati kinanda kimepapaswa na Kalikiti Moto.

Kazi hii maridadi imerekodiwa katika studio za Sofia Records chini ya producer Ababuu Mwana Zanzibar.

Wimbo huu ni sehemu ya nyimbo zitakazounda albam ya “Sura Surambi” itakayozinduliwa rasmi Alhamisi ya Novemba 26 mwaka huu pale Mango Garden Kinondoni.

Pata uhondo hapo juu kwa kuusikiliza wimbo huo “Pendo la Ukakasi” kutoka kwa Saida Ramadhan.

CHALLENGE CUP: KIBADENI ATAJA SILAHA 21 ZA KILIMANJARO STARS

$
0
0


Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini Ethiopia.
Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya mazoezi na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.
“Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika” amesema Kibadeni.
Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).
Viungo Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga), washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).
Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.
Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha Taifa Stars.
Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi, Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.



YVONNE NELSON ASEMA ROHO ZA KOROSHO ZA WASANII ZINAUA FILAMU GHANA

$
0
0


SUPASTAA wa Ghana, Yvonne Nelson, amesema medani ya filamu nchini humo inashindwa kupiga hatua kutokana na wivu wa wasanii.
Akizungumza na kituo cha Suncity 97.1 Radio cha Ghana, Yvone alisema, wasanii wengi wa Ghana hawapendani na pia hawapendi maendeleo ya wengine.

MKUBWA FELLA SASA APANGA KUMNG’ARISHA KAYUMBA BSS

$
0
0


MNENE wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella amesema kuwa, baada ya chipukizi wao, Kayumba Juma kuibuka mshindi wa shindano la BSS, hivi sasa wanajiandaa na mipango ya kujua nini wafanye ili kumng’arisha.

Akiongea na Saluti5, Fella alisema kuwa, wanachosubiri kwa muda huu kabla ya kuanza mikakati hiyo, ni wandaji wa shindano hilo kumalizana nae kwa kumlipa haki zake za ushindi.

“Kayumba tuko nae zaidi ya miaka miwili hivi sasa hapa Mkubwa na Wanawe na binafsi nilifikiri bado hajakomaa, lakini kwa vile keshafika hatua hii ya ushindi wa BSS, hakuna namna nyingine ni ‘kumtoa’ tu,” alisema Fella.

Katika shindano la BSS la mwaka huu, licha ya changamoto nyingi ikiwamo kujitokeza kwa vijana wengi wenye vipaji, Kayumba alifanikiwa kuibuka kuwa mshindi na kuleta faraja ndani ya Mkubwa na Wanawe. 

MADEMU WA FLAVOUR WACHACHAMAA, WATAKA AWAOE WOTE PAMOJA

$
0
0


MSANII maarufu wa Hiphop nchini Nigeria, Chinedu Okoli maarufu kama Flavour, amelazimishwa na wanawake wote aliozaa nao awaoe.

Flavour alizaa na wanawake wawili kwa nyakati tofauti na bada ya kutangaza kwenye kituo kimoja kwamba amekaribia kuoa, wanawake hao wameungana na kutaka awaoe wote.

“Ninataka kuoa hivi karibuni ili nipate kutulia na kuendeleza muziki wangu,” alikiambia kipindi cha ‘Golibe Crooner’ ndani ya Hip Tv.

Flavor ambaye ni rapa mzaliwa wa jimbo la Enugu, baada ya kutangaza nia ya kuoa, wanawake alioza nao; Sandra Okagbue na mwanamitindo Anna Banner, wamemtaka awaoe kabla hawajamwanzishia kasheshe.

MKE WA 2FACE ANYOA UPARA KUPIGA VITA UGONJWA WA KANSA

$
0
0

MSANII Annie Idibia ambaye ni mke wa mwanamuziki maarufu barani Afrika, 2face Idibia, amenyoa nywele zake katika jitihada za kupiga vita ugonjwa wa kansa.

Annie ambaye kuanzia Oktoba, mwaka huu amekuwa balozi wa kupiga vita ugonjwa wa kansa, amewataka wanawake kupima mara kwa mara ili kuepuka hatari ya ugonjwa huo.

Aliandaa hafla iliyowausisha wasanii kibao kama Chioma Akpota, Chidinma Ekile na wengine wengi.

VANESSA MDEE AKUMBUKA ALIVYOUZA VOCHA NA KUSAJILI LAINI ZA SIMU KABLA HAJAWA MAMBO SAFI

$
0
0


STAA wa kike wa Bongofleva, Vanessa Mdee amesema kuwa, amewahi kufanya biashara ya kuuza kadi za simu na laini pale alipohitimu kidato cha nne.

Alisema kuwa, wakati anamaliza kidato cha nne, aliajiliwa kwenye kampuni ya simu na kupangiwa kusajili na kuuza laini zenye jina la kampuni hiyo akiwa jijini Arusha.

“Nashukuru Mungu hapa nilipofika kwani nilipotoka ni mbali sana, nilishawahi kukuza laini na kusajili namba maalum (special number) za watu nikiwa Arusha, lakini sasa maisha safi nasafiri nchi yoyote nitakayo kwa dakika chache,” alisema.

Vanessa anayefahamika pia kama ‘Vee Money’ alisema kuwa anaamini mafanikio yake yametokana na juhudi binafsi, ambapo nadai hakuwahi kukata tamaa kwasababu alijua Mungu yupo pamoja naye.

Aliwaomba mashabiki wake kutokata tamaa na kuendelea kujituma na kupambana kwa nguvu ili kupata mafanikio.


ZINADINE ZIDANE AANZA KUMKATIA TAMAA CRISTIANO RONALDO REAL MADRID

$
0
0
NGULI wa klabu ya Real Madrid, Zinadine Zidane amesema uwezekano wa mshambuliaji mahiri wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo (pichani) kwenda Paris saint-Germain (PSG) ya Ufaransa, ni mkubwa.

Zidane aisema, anahisi rais wa Real Madrid, Florentino Perez atakubaliana na maombi ya kila wakati kutoka kwa rais wa PSG, Nasser El Kheraifi.

Aliema, namna ambavyo PSG wanamtaka Ronaldo mwenye miaka 30 na Karim Benzema ni ngumu kuwazuia na kwa mtazamo wake anadhani ni bora kuwauza.

“Kwa jinsi ilivyo Ronaldo na Benzena wana uwezekano mkubwa wa kuondoka Real sasa kuliko wakati wowote mwingine,” alisema Zidane
“Lakini sifikirii kama itakuwa busara kumuuza Gareth Bale pamoja nao hata kama itakuja ofa nono, kwa kuwa huyu ni mchezaji ambaye bado tunamhitaji sana, Santiago Bernabeu,” aliongeza Zidane.

Zidane, mkurugenzi wa soka anayehusudiwa na kuheshimiwa sana na mashabiki wa klabu hiyo, alisema kwa asa kila mmoja ameingiwa na woga wa kuwapoteza washambuliaji hao wawili kutokana na mikakati na msimamao wa Nasser El-Khelaifi.

Alisema, inavyoonekna bilionea wa PSG raia wa Qatar, hivi sasa amejipanga kuwa na Ronaldo, hivyo ametenga dau ambalo ni vigumu kilikataa.

“Tungali na mkataba na Ronaldo, naamini hatalazimisha kuvunja, lakini akiamua hivyo hatutakuwa na namna zaidi ya kuheshimu maamuzi yake,” aliafafanua.

CARLO ANCELOTTI HAIFAGILII BARCELONA

$
0
0
Ronaldo's relationship with Carlo Ancelotti was strong and he supported the boss up until his sacking
KOCHA Carlo Ancelotti amesema hajawahi kutamka kuwa timu ya Barcelona ni nzuri kuliko nyingine.

Ancelotti amedai hajawahi kuzungumza hivyo na kueleza kwamba anashangaa taarifa hizo zimetoka wapi.

Alisema ana imani kwamba waandishi hawakumsikia vizuri, kitu ambacho kimesababisha kuandika habari ambazo si za kweli.

“Mimi sijasema kwamba Barca ndio timu bora ulimwenguni, sijui wameipata wapi taarifa hiyo,” alisema.

KOCHA BRAZIL MAPIGA CHAPUO NEYMAR KUWAPIKU MESSI NA RONALDO

$
0
0

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amemuonya nahodha wake, Neymar Jr akimtaka kuongeza bidii uwanjani ili awapiku Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Dunga alisema jna kwamba, imefika wakati kwa mchezaji huyo wa Brazil kuonyesha kwamba ana uwezo mkubwa kuliko nyota hao.

Alisema, ana imani uwezo wa Neymar ni mkubwa sana kama ataongeza bidii ya kufanya mazoezi na kujifunza mambo zaidi kutoka kwa Ronaldo na Messi.

“Hawa ni wachezaji wazuri, lakini bado nina imani kwamba anatakiwa kuongeza bidii ya kutosha ili aweze kufunga mabao zaidi,” alisema.

GARRY NEVILLE AIONYA MANCHESTER UNITED JUU YA USAJILI WA RONALDO, ASEMA NI BORA KUTENGA PESA KWA GARETH BALE

$
0
0
Ronaldo is not overly impressed with Gareth Bale (left) being the 'centre-piece' of a new-look Madrid side
Beki wa zamani wa Manchester United, Garry Neville ameitaka klabu hiyo kuachana na ndoto za kumsajili Ronaldo, badala yake amewataka kuelekeza nguvu zao kwa Gareth Bale.

Garry Neville ambaye pia alikuwa nahodha wa zamani wa United, alisema kwa mtazamo wake, Bale atakuwa na faida mno iwapo atasajiliwa na klabu hiyo kuliko itakavyokuwa wakimrejesha Cristiano Ronaldo.

Staa huyo wa zamani amemtaka kocha wa United, Louis Van Gaal, kuwa makini katika suala zima la usajili asikimbilie majina bali aangalie manufaa ya mchezaji anayemuhitaji.

Kauli ya Neville imekuja baada ya kocha wa Man United, Louis Van Gaal kusemekana kuwa na mpango wa kumrejesha nyota wa Real Madrid kwenye klabu hiyo ya Old Trafford wakati wa majira ya joto yajayo.

Ronaldo aliondoka Ligi Kuu ya Englanda na kwenda Hispania mwaka 2009, kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia - pauni mil. 80, kabla ya Bale kuvunja rekodi hiyo miaka minne baadae.

Hata hivyo, mwanasoka huyo mstaafu, Neville alisema kuwa ana shaka kama Mreno huyo atarejea Man United na anaweza kufanya vizuri.

“Sina uhakika kama kitakuwa kitu kizuri kwa Cristiano kurejea Man United,” Neville aliliambia gazeti la The Mirror.

DROGBA AZUNGUMZIA UWEZEKANO WA KUICHEZEA TENA CHELSEA

$
0
0
Drogba has scored 12 goals in as many games since he joined Montreal Impact in July
STRAIKA Didier Drogba amekana kuwa, wakati atakapoutumia muda wake akiwa jijini London kwa mapumziko ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), kutamfungulia njia ya kucheza tena Chelsea.

Msimu uliopita nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 alipewa nafasi ya kucheza kwa mara ya pili kwenye klabu hiyo ya Stanford Bridge, kabla ya kuhamia timu ya Montreal Impact inayocheza igi hiyo ya MLS.

“Kuchezea tena Chelsea? Kwa sasa sina mawazo hayo,” Drogba aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP). “Nahitaji kupumzika na kuhakikisha nipo tayari kwa ajili ya msimu mpya.”

KOCHA WA ENGLAND ASEMA HABABAISHWI NA KIPIGO CHA HISPANIA

$
0
0
The England boss admits the Paris terror attacks will be 'lingering over everybody' at Wembley on Tuesday
KOCHA mkuu wa England, Roy Hodgson amewataka wachezaji wa timu hiyo kutovurugwa na kichapo cha juzi kutoka kwa Hispania, ambacho ni cha kwanza katika miezi 17 iliyopita.

England ambayo haijapoteza mchezo wowote katika michezo ya kufuzu mashindano ya Euro 2016, ilikumbana na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Hispania katika mchezo wa kirafiki, huku mabao hayo yakitupiwa wavuni na Mario Gaspar na Santi Cazorla.

Hata hivyo, Hodgoson aliitaka timu hiyo kuachana na matokeo hayo na badala yake kuhakikisha haipotezi hali ya kujiamini na kufanya vizuri katika michezo ijayo.

“Unapopoteza mchezo kwa mara ya kwanza, jambo muhimu ni kuhakikisha haupotezi hali ya kujiamini,” alisema Mwingereza huyo.

Kikosi hicho kilishuka dimbani bila ya kinara wa mabao Premier League, Jamie Vardy ambaye ni majeruhi na anaweza kukosa pambano dhidi ya Ufaransa, mchezo utakaochezwa kesho kwenye dimba la France Wembley Stadium nchini England.

UNAJUA SIFA ZA NDEGE ALIYONUNUA RONALDO?

$
0
0
Cristino Ronaldo sees the funny side as he is interviewed by Jonathan Ross on the presenter's show
Hivi majuzi mshambuliaji wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo, alinunua ndege ya kifahari kwa euro mil. 19.

Taarifa iliyotolewa na gazeti la Correo da Manha la Ureno, imeeleza kwamba mchezaji huyo amenunua ndege hiyo hivi karibuni ambayo ina sifa zifuatazo:

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba watu wanane hadi 10 kwa wakati mmoja, ambapo kuna chumba cha kupika na chumba cha kupumzika.


Pia ina sehemu ya mkutano na vyoo viwili vya abiria na marubani, ambapo ndege hiyo imefahamika kuwa ni ya aina ya Gulfstream.
Hii ndiyo ndege ya Ronaldo



LUIS FIGO AMTAKA JOSE MOURINHO AIFUMUE CHELSEA

$
0
0
  Mourinho takes his Chelsea team back to Portugal to face Porto in the Champions League on Tuesday
NYOTA wa zamani Luis Figo amemtaka kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kukifanyia marekebisho kikosi chake ambacho kimeonyesha kiwango kibovu kilichowafanya wafungwe mechi saba kati ya 12 za mwanzo wa Ligi Kuu England.

Kwa sasa kikosi hicho cha Mourinho kipo nafasi ya 16, kikiwa na pointi 11, huku kikiwa kimepoteza mechi tatu za mwisho kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za timu ya taifa.

Hadi sasa mabingwa hao watetezi wapo nyuma kwa pointi 15 dhidi ya timu zinazoongoza Ligi hiyo, Manchester City na Arsenal na hatima ya Mourinho kuendelea kuinoa klabu hiyo ya Stamford Bridge ipo shakani.

Hata hivyo, Figo ambaye amewahi kufundishwa na Mourinho, anaamini kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 anaweza kuifanya Chelsei kuzinduka.

“Nadhani maisha ya kocha ni kama haya,” alisema staa huyo wa zamani na kuongeza:.“Matokeo sio mazuri, lakini hutakiwi kumlaumu kocha.”

ARJEN ROBBEN AANZA KUWAZA MAISHA NJE YA TIMU YA TAIFA YA HOLLAND

$
0
0
Holland captain Arjen Robben (left) is all smiles after scoring his second goal against Wales in the 3-2 victory on Friday night 
KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama kaanza kukata tamaa, staa wa Bayern Munich, Arjen Robben amesema kwamba anavyodhani tayari ameshaichezea timu yake ya taifa ya Uholanzi mashindano ya mwisho ya kimataifa.

Bada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka jana, Uholanzi pia imeshindwa kufuzu fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2016 baada ya kushika nafasi ya nne katika michuano ya kufuzu fainali hizo hatua ya makundi.

Kutokana na hali hiyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, anaamini kwa kushindwa namna hiyo, kunaweza kumkatisha tamaa mchezaji yeyote anayeichezea timu ya taifa.

“Kushindwa kufuzu fainali za Euro 2016, kumeathiri moyo wa kila mmoja wetu,” Robben aliliambia jarida la Metro News.

“Pengine nimeshacheza mechi zangu za mwisho katika mashindano ya kimataifa,” alisema nyota huyo.


Hata hivyo alisema kuwa pengine anaweza kufanya hivyo kama watafuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 kama atakuwa hajastaafu kucheza soka.

KOCHA DIEGO SIMEONE SASA AHUSISHWA NA CHELSEA

$
0
0
Diego Simeone believes his side are back on track after failing to retain their La Liga title last season
KLABU ya Chelsea inamfuatilia kwa karibu Diego Simeone ili kurithi mikoba ya Mreno Jose Mourinho, wakati huu ambao Muargentina huyo anaangalia jinsi ya kuondoka Atletico, Madrid mwishoni mwa msimu.

Mbali na kocha huyo, Chelsea pia inawafikiria kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers, Roberto Di Matteo na Guus Hiddink.

Uamuzi huo umekuja ikiwa ni baada ya Chelsea kudorora msimu huu, ikiwa imepoteza mechi saba kati ya 12 za Ligi Kuu England, ikishinda tatu ytu na kupata sare mbili.

Hali hiyo imewafanya kuwa katika nafasi ya 16 baada ya kujikusanyia pointi 11 ndani ya mechi 12, huku Manchester City ikiwa kileleni na pointi zao 25, sawa na Arsenal na Leicester City zinazotofautiana kwa mabao.

DOGO RAMA, KUPAZA, JOJOO JUMANNE WAACHANA RASMI NA TWANGA PEPETA …wajiunga na Double M Sound ya Muumin

$
0
0

Baada ya danadana za wiki kadhaa, hatimaye Mwimnjuma Muumin amewanyakua rasmi waimbaji Dogo Rama na Saleh Kupaza kutoka Twanga Pepeta na kuwasajili kwenye bendi yake ya Double M Sound.

akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Equator Grill, Mtoni jijini Dar es Salaam mchana huu, Muumin alisema waimbaji hao sasa ni mali ya Double M Sound na kinachofuata ni ujio wa nyimbo mpya za kufunga mwaka.

Sambamba na waimbaji hao wawili, Muumin pia ametangaza kumchukua mpiga bass wa Twanga Pepeta Jojoo Jumanne.

Wanamuziki hao watatu wakizungumza katika kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari, wakasema sababu kubwa inayowatoa Twanga Pepeta ni madai ya kulimbikiziwa mishahara yao.

“Hatujalipwa mishahara kwa miezi mingi sana na hakuna sababu za msingi zinazotolewa,” walisema Dogo Rama na Kupaza.


Jojoo Jumanne akasema ana madai mengi sana kwa Twanga Pepeta ambayo haitaji kuyaweka wazi zaidi ya kuamua kwenda kusaka changamoto mpya.

Picha za mkutano huo wa waandishi wa habari zitakujia baadae.

PICHA 10 ZA DOGO RAMA, KUPAZA NA JOJOO JUMANNE WAKITAMBULISHWA KUJIUNGA NA DOUBLE M SOUND

$
0
0

Bendi ya Double M Sound ya Mwinjuma Muumin leo ilifanya mkutano na waandishi wa habari kutambulisha wasanii wake wapya.

Wasanii hao ni waimbaji Saleh Kupaza, Dogo Rama na mpiga bass Jojoo Jumanne wote kutoka Twanga Pepeta.


Zifuatazo ni picha 1o za mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika Equator Grill Mtoni jijini Dar es Salaam.
Mkutano wa Double M na waandishi wa habari ukiendelea
Kutoka kushoto ni Dogo Rama, Muumin, Kupaza, Jojoo Jumanne na Rashid Sumuni katika mkutano wa waandishi wa habari
 Wasanii wa Double M Sound
Omar Kisila mpiga kinanda wa Double M Sound
 Kulia ni mbiga bass Jojoo Jumanne kutoka Twanga
 Wasanii wa Double M wakiwapa burudani wanahabari
Burudani ikiendelea
Mkurugenzi wa Double M Mwinjuma Muumin akisisitiza jambo
 Double M Sound ikinadi wasanii wake wapya
Dogo Rama, Muumin, Kupaza



Viewing all 8805 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>