Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live

FRANK DE BOER APIGIWA DEBE EVERTON

$
0
0
FRANK de Boer ndie mtu sahihi kuifundisha klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya England.

Kaka wa Frank, Ronald de Boer aliliambia gazeti moja kuwa: “Sio jukumu lake, hiyo ni kwa ajili ya klabu na maendeleo kwa ujumla.”

Everton waliwahi kumuhitaji kocha wa Southampton, Ronald Koeman Rafael Benetez anayeifundisha Newcastle United.
Lakini Danny Mills, beki wa zamani wa England alisema kwamba Benetez alistahili.

Everton imemaliza mechi zake ikiwa nafasi ya tano, imejikusanyia pointi 72.


Roberto Martinez, kocha aliyetimuliwa ndie alipewa mikoba ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa David Moyes mwaka 2013.

RAHA ZA TWANGA PEPETA ZAREJEA MANGO GARDEN USIKU HUU

$
0
0

Baada ya kukosekana kwenye ukumbi wao wa nyumbani wa Mango Garden kwa Jumamosi mbili mfululizo, Twanga Pepeta leo usiku wanarejea kwenye kiwanja hicho cha watoto wa mjini.

Bendi hiyo ilikosekana Mango wiki mbili zilizopita kufuatia ziara za mikoani, lakini wiki hii meneja wa Twanga Pepeta Hassan Rehani ameithibitishia Saluti5 kuwa bendi yao ipo Mango Garden Jumamosi hii.

Twanga Pepeta wanatarajiwa kukata kiu ya mashabiki wao kwa nyimbo zao kali zikiwemo zile mpya kabisa “Mtu Makini”, “Twanga Kwanza” ambazo zinachagizwa na rap tamu ya “Banjuka”.

LOUIS VAN GAAL APIGA HESABU KALI ZA KUBAKIA MANCHESTER UNITED

$
0
0
Manchester United are recruiting for a 'scouting auditor' to help improve their scouting department

LOUIS VAN GAAL amekubali kuwa Manchester United itakuwa imefeli kama itashindwa kufuzu kwa Champions League, lakini akasisitiza kuwa bado ana matumaini ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo msimu ujao.

United inahitaji kushinda dhidi ya Bournemouth Jumapili na kuomba Manchester City ipoteze mbele ya Swansea, kama inataka kufuzu kwa Champions League.

Kufeli kufuzu kwa Champions League kulimgharimu David Moyes miaka miwili iliyopita na tayari uvumi unazagaa kwa kasi kubwa kwamba Van Gaal anaweza kufuata nyayo zake na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.

Lakini kocha huyo Mholanzi hajakata tamaa kwani bado ana matumaini ya kufanya vizuri na kuendelea kubaki Old Trafford: "Tunaweza kushinda FA Cup. Wangapi bado wapo kwenye mbio hizo (kuwania FA Cup)? Si wengi.

“Bila shaka tusipofuzu kwa Champions League hatutaweza kufikia lengo letu. Lakini tupo katika fainali ya FA Cup na tupo katika mbio za mechi ya mwisho (ya Premier League)… kimahesabu bado tunaweza kufuzu. Ni klabu ngapi zinaweza kusema hivyo?

"Bila shaka unaweza kusema Manchester United inahitaji kuwa bingwa – ndiyo, najua matarajio ni hayo, lakini sidhani kama ni ukweli. Na nimesema nitakuwa hapa, hayo ni maoni yangu, hivyo bodi itaamua kama itapenda kuwa hivyo.”

KOCHA QUIQUE WA WATFORD ATOA MKONO WA BAIBAI

$
0
0

IMEFAHAMIKA kwamba kocha Quique Sanchez Flores, ataondoka Watford baada ya mechi ya mwisho.
Watford inatarajia kucheza mechi yake ya mwisho keshokutwa.

Sanchez, raia wa Hispania mwenye miaka 51 aliteuliwa Juni, mwaka jana kuchukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo baada ya kufanikiwa kupanda daraja.

Watford inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, imeshinda mechi mbili tu kati ya 11 ilizocheza ugenini.

Sanchez aliyeiongoza Watford kucheza nusu fainali ya Kombe la FA msimu huu, ataondoka baada ya mechi yao na Sunderland.

“Tuna kila sababu ya kumshukuru Quique. Yeye na wataalamu wenzake wamefikia malengo yetu ya kubaki kwenye Ligi Kuu kwa mwaka wa pili,” ilieleza taarifa ya klabu.

“Quique anaondoka akiwa na baraka zetu zote tukimtakia mafanikio aendako, mawazo yake bado tunayahitaji, asisite kufanya hivyo.”

Mwezi uliopita klabu hiyo ilisema ingeujadili mustakabali wa kocha huyo baada ya msimu kumalizika.

Watford inamsaka kocha wa saba tangu iliponunuliwa na familia ya Pozzo ambao wanamiliki timu ya Udinese ya Italia.

KANTE WA LEICESTER CITY NDANI YA KIKOSI CHA UFARANSA EURO

$
0
0
KIUNGO Leicester City, N’Golo Kante ametajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016.

Michuano ya mwaka huu itachezwa nchini Ufaransa na tayari nchi mbalimbali zinaendelea na maandalizi.

Kante (25), alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango mkubwa ndani ya Leicester City na kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa England msimu huu.

Mchezo wake wa kwanza kuichezea Ufaransa ulikuwa dhidi ya Uholanzi uliochezwa Machi, mwaka huu.

Kante ni mmoja kati ya wachezaji 10 wanaocheza Ligi Kuu ya England walioitwa katika kikosi cha UEkienachoenoeleewa na Didier Deschamps.

Lakini mshambuliaji aliye kwenye kiwangoHatem ben Arfa na MathieuValbuena anayehusishwa na kashfa ya kurekodi mkanda wa ngono na mchezaji mwenzake wa kimataifa, Karim Benzema, wameachwa.

Arfa ni miongoni mwa wachezaji wanane waliowekwa benchi, akiwemo kiungo wa Manchester United, MorganSchineiderlin na mshambuliaji wa Lyon, Alexandre Lacazette.


Benzema, mshambuliaji wa Madrid anachunguzwa kwa kashfa hiyo ingawa amejulhihshwa kwamba atakuwemo katika kikosi cha Ufaransa.

BARCELONA YATWAA UBINGWA HISPANIA ...Luis Suarez moto chini, Ronaldo apiga 2 lakini Real Madrid yaishia nafasi ya pili

$
0
0
Barcelona imetwaa taji la La Liga baada ya kuifunga Granada 3-0 katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Hispania.

Hiyo inakuwa ni mara ya 24 kwa Barcelona kufanya hivyo, safari ikiwa ni kwa msaada mkubwa wa mshambuliaji Luis Suarez  ambaye katika mchezo huo wa mwisho alipachika mabao yote matatu.

Real Madrid iliyokuwa inasubiri Barcelona iteleze, imeishia nafasi ya pili licha ya kuifunga Deportivo La Coruna 2-0, mabao yote yakifungwa na Cristiano Ronaldo.
Luis Suarez leaps into the air to celebrate doubling Barcelona's lead as they secured a second La Liga title in a row on Saturday
Luis Suarez akiruka juu kushangilia goli lake la kwanza
The former Liverpool striker continued his prolific season in front of goal as his first-half double inspired Barca to victory over Granada
Suarez alifunga magoli yote matatu ya Barcelona
Suarez celebrates scoring for Barcelona on another dominant day for the Catalan giants as they retained the Spanish league title
Suarez akishangilia moja ya mabao yake
Lionel Messi and Jordi Alba join in the celebrations as Barcelona neared their third league title in the last four seasons
Lionel Messi na Jordi Alba wakishangilia baada ya Barcelona kutwaa ubingwa 

HIVI NDIVYO BAYERN MUNICH WALIVYOAGANA NA KOCHA PEP GUARDIOLA

$
0
0
Pep Guardiola gets his hands on the trophy before he leaves the German giants after three-and-half years in charge

Baada ya misimu mitatu, Pep Guardiola ameiaga Bayern Munich kwa shangwe za aina yake baada ya mchezo wa mwisho wa Bundesliga ulioisha kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Hannover.  

Guardiola anaondoka Bayern huku akiwa na mataji matatu ya Bundesliga aliyoyavuna katika kila msimu lakini hakubahatika kuipa ubingwa wa Champions League klabu hiyo ya Ujerumani.

Mara baada ya mchezo huo uliofanyika Allianz Arena na kukabadhiwa rasmi taji lao, wachezaji wa Bayern Munich wakashangilia kwa staili ya kumtotesha kocha wao mwili mzima kwa bia. 

Guardiola ambaye kabla hajajiunga na Bayern, alikuwa kocha wa Barcelona, msimu ujao atakuwa bosi wa Manchester City.

David Alaba throws the contents of a Weißbier (three litre beer glass) over outgoing Bayern Munich manager Pep Guardiola
David Alaba akimmininia bia kocha wa Bayern Munich  Pep Guardiola baada ya mchezo wa mwisho dhidi ya Hannover
Douglas Costa joined his Bayern team-mate as the pair interrupted photographs of Guardiola and his coaching staff to drench them with beer
Douglas Costa akiungana na wachezaji wenzake wa Bayern kumwaga kocha Guardiola kwa staili ya aina yake
Guardiola, who will take charge of Manchester City in the summer, won three Bundesliga titles but failed to win the Champions League
Guardiola, ambaye msimu ujao atakuwa kocha wa Manchester City ameshinda mataji matatu ya Bundesliga lakini ameshindwa kutwaa ubingwa wa Champions League akiwa na Bayern Munich

MASHAUZI CLASSIC KUVAMIA MTWARA, MASASI, NACHINGWEA NA LINDI MWISHONI MWA MWEZI HUU

$
0
0

Kundi la Mashauzi Classic Modern Taarab litavamia miji ya Nanchingwea, Masasi, Mtwara na Lindi mwishoni wa mwezi huu katika maonyesho maalum ya vunja jungu.

Alhamisi ya tarehe 26 mwezi huu Mashauzi Classic wataanzia Nanchingwea ndani ya NR (Nachingwea Resort), siku itakayofuata Ijumaa Mei 27 kundi hilo litahanikiza burudani zao Masasi katika ukumbi wa Emirates.

Meneja wa Mashauzi Classic Ismail “Sumaragar” ameiambia Saluti5 kuwa Jumamosi Mei 28 kundi lao lituwa Mtwara mjini kwenye ukumbi wa Fire na Jumapili Mei 29 watamalizia ziara yao ya kusini katika mji wa Lindi ndani ya ukumbi wa Bwalo la Polisi.

MANUEL PELLEGRINI ‘AAGA’ MAN CITY HUKU AKIMUONYA PEP GUARDIOLA

$
0
0
Pellegrini is confident that City can finish in the top four and qualify for the Champions League next season
MANUEL PELLEGRINI amemuonya Pep Guardiola kwamba anaweza kuwa katika mshtuko wa kufanya vibaya wakati atakapofanya kazi kwa mara ya kwanza katika Premier League msimu ujao.

Kocha huyo ataiongoza Manchester City katika mechi yake ya mwisho Jumapili, akihitaji walau pointi moja nyumbani kwa Swansea City kuweza kufuzu Champions League kwa ajili ya mrithi wake Guardiola, ambaye atachukua nafasi yake kiangazi hiki.

Pellegrini anaamini kwamba kocha huyo wa Bayern Munich atakuwa amejiandaa vizuri awezavyo kwa maisha ya England na anatarajia Mhispania huyo atakuwa na mafanikio.

Hata hivyo, alisema kwamba makali ya Premier League ni tofauti na mengine ambayo Guardiola ana uzoefu nayo, na akakiri kuwa yeye ilimchukua muda kukaa sawa wakati alipojiunga na City miaka mitatu iliyopita.


Pellegrini alishinda mechi moja tu kati ya sita za mwanzo za ugenini katika msimu wake wa kwanza kabla ya kuiongoza City kushinda taji la Premier League.

HILI NDIO KOSA ANALOJUTIA SIR ALEX FERGUSON KATIKA UKOCHA WAKE MANCHESTER UNITED

$
0
0
Carlo Ancelotti met with Sir Alex Ferguson in 2013 and the Italian was offered the Manchester United job

SIR ALEX FERGUSON ameshinda mataji 28 katika miaka yake 27 ya kuwa kocha wa Manchester United, lakini pamoja na mafanikio hayo, amekiri kuwa uamuzi wake wa kutangaza kustaafu mwaka 2001 ni kosa kubwa kuliko yote aliyopata kuyafanya akiwa na timu hiyo.

Mkongwe huyo wa miaka 74 anayetambulika kama “kocha mkubwa” katika historia ya soka, alistaafu rasmi mwaka 2013, lakini miaka 12 kabla kuchukua uamuzi huo, alipanga kuondoka Old Trafford akiwa na umri wa miaka 60.

Tofauti na mwaka 2013 wakati alipoishtua dunia ya soka na tangazo lake la kustaafu mwisho wa msimu, mwaka 2001 Sir Alex aliutangazia umma kustaafu mwanzo wa msimu na anakiri kuwa lilikuwa kosa kubwa zaidi.


 “Kosa kubwa nililofanya ilikuwa kutangaza hilo mwanzo wa msimu… Lilikuwa kosa, na mke wangu na wanangu watatu walibadili mtazamo wangu kuelekea jambo hilo mwezi Januari na nikaanza kufikiria tena kuhusu United,” alisema.

GRANIT XHAKA ATAKA UHAMISHO WAKE KWENDA ARSENAL UKAMILIKE KABLA YA EURO 2016

$
0
0

NYOTA anayelengwa na Arsenal katika usajili wa kiangazi hiki, Granit Xhaka amesema kuwa ana matumaini uhamisho wake utafanikishwa kabla ya kuanza fainali za michuano ya mataifa ya Ulaya - Euro 2016.

Xhaka – nyota wa kimataifa wa Uswisi amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Arsenal katika siku za karibuni, huku ripoti zikisema kuwa ofa ya pauni milioni 33.8 tayari imewekwa mezani.

Hata hivyo, wakati kiungo nyota wa Leicester City, N’Golo Kante akionekana pia kuwa lengo kuu la Arsene Wenger, Xhaka anaonekana “kuitia mzuka” Arsenal kuharakisha kukamilisha dili la kumpeleka Emirates.

 “Nitakuwa na furaha kama kila kitu kitatatuliwa kabla ya Michuano ya Ulaya,” alisema kiungo huyo wa miaka 23 kuwambia waandishi wa habari.


“Itakuwa vizuri kwangu kama ninakwenda katika mashindano yale makubwa bila kuwa na wasiwasi katika mawazo yangu.”

CHAZ BABA NA CHOKORAA SASA HAWAKAUKI TWANGA PEPETA … mmoja wao yu njiani kurejea nyumbani

$
0
0

Waimbaji nyota wa zamani wa Twanga Pepeta, Khalid Chokoraa na Chaz Baba kwasasa wamekuwa  wakionekana mara kwa mara kwenye maonyesho ya Twanga hususan yale yanayofanyika Mango Garden Kinondoni siku za Jumamosi.

Kila wanapokuwa hawana kazi kwa siku hiyo, waimbaji hao wamekuwa wakienda kuchungulia bendi yao ya zamani na wakati mwingine kupanda kabisa jukwaani na kushiriki kuimba baadhi ya nyimbo walizoziimba enzi hizo wakiwa na Twanga Pepeta.

Jana Jumamosi waimbaji hao walionekana Mango Garden ambako Chokoraa alibakia kama mtazamaji wakati Chaz Baba yeye alipanda jukwaani na kuimba wimbo “Mwana Dar es Salaam.

Chaz Baba akashangiliwa na mashabiki wa Twanga huku wengine wakienda kumtunza mshiko wa maana.

Chokoraa yuko na Mapacha Watatu, Chaz Baba ni mtumishi wa Mashujaa Band lakini kwa sasa kuna tetesi kubwa ambazo zimepenyezwa Saluti5 kuwa mmoja wao yuko njiani kurejea Twanga Pepeta.

Chanzo kimoja cha Saluti5 kimesema onyesho kubwa linaandaliwa kabla ya mapumziko ya  mwezi mtukufu wa Ramadhan kwaajili ya kutambulisha ujio rasmi wa mmoja wa waimbaji hao wawili.

"JIAMINI" WA ISHA MASHAUZI WAWEKA REKODI MPYA TOP TEN YA TK FM YA TANGA ...wakamata no.1 kwa wiki ya 6 mfululizo

$
0
0


Wimbo wa “Jiamini” wa Isha Mashauzi umeendelea kushika namba namba katika chati hizo za radio TK FM ya Tanga kwa wiki ya sita mfululizo.

TK FM (Tanga Kunani) kwa sasa ndiyo radio yenye mashabiki wengi zaidi katika mji wa Tanga huku moja ya vipindi vyake bomba ni Afro Dancee inayopiga nyimbo za dansi za Tanzania na kwingineko barani Afrika.

Wimbo “Jiamini” ambao ni project binafsi ya Isha Mashauzi nje ya muziki wa taarab, umevunja rekodi ya wimbo “Moyo Wangu” wa FM Academia ambao ulikamata namba moja kwa wiki tano mfululizo.

Chati hizo huwekwa hadharani kila siku za Ijumaa kupitia kipindi hicho cha Afro Dance kinachoruka kila siki (kasoro Jumamosi) kuanzia saa saa 2.10 usiku hadi saa 4 usiku chini ya mtangazaji Rodger Kiss.

Kabla ya kukamata namba moja, Jiamini iligota kwenye nafasi ya pili na ya tatu kwa muda mrefu.

Itazame chati hiyo hapo chini ili kupata nyimbo bora 1o kwa wiki iliyopita.



VAN GAAL AFUNGUKA NA KUSEMA ATAENDELEA KUBAKIA MANCHESTER UNITED

$
0
0
LOUIS Van Gaal anafikiri bado ataendelea kuwa meneja wa Manchester United msimu ujao.

Mholanzi huyo hajapewa uhakika wowote kwenye hatma yake ya baadae, lakini anatarajia kulinda mwaka wake wa mwisho uliobakia katika mkataba wake wa miaka mitatu aliousaini mwaka 2014.

Alisema: “Nimesema nitakuwepo hapa, hayo ndiyo maoni yangu, hivyo bodi inaweza kuamua kama ni hilo au la.”

Van Gaal amekuwa chini ya shinikizo kubwa tangu Desemba na meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho  anajulikana alishazungumza na maofisa wa United.

 United ambao walitangaza rekodi ya robo ya tatu ya matokeo juzi Ijumaa na kusema wanatarajia kwa ujumla mapato kupita pauni mil. 500 kwa mwaka, wanajua wataikosa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili katika misimu mitatu kama Manchester City wataepuka kushindwa katika mechi yao na mwisho na Swansea.

Huku wakiwa na uhakika wa kucheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Crystal Palace hapo Mei 21, Van Gaal amesema kuchukua vita kwa ajili ya nafasi ya nne kwa mchezo wa mwisho inawakilisha shahada ya mafanikio.

“Tunaweza kushinda Kombe la FA,” alisema “Na sisi bado tupo katika mbio. Ni timu ngapi unaweza kusema hilo? Si nyingi. Lengo letu ni kufuzu. Bila ya shaka unaweza kusema Manchester inahitaji kuwa mabingwa, ndiyo najua matarajio ni kama hayo, lakini si kufikiria kuwa ni kweli.”

Van Gaal mara kwa mara amerejea madai yake kwamba vyombo vya habari ‘vilishamtimua’ miezi sita iliyopita.
Kama anabakia au la, Van Gaal tayari ameshiriki kikamilifu katika mipango ya kampeni za 2016/17, akipunguza ziara ya kujiandaa na msimu mpya kwa siku sita kamili na mechi mbili nchini China.

Pia anajua eneo analohitaji kuimarisha baada ya kutolewa nje katika mpango wa uwezekano wa dili kwa Renato Sanches aliyejiunga na Bayern Munich kutoka Benfica juzi.

“Sidhani tuna kuboresha sana,” alisema. “Lakini tunahitaji haraka wachezaji wabunifu katika kushambulia. Hiyo ni kile nilichosema kabla ya msimu huu.”


Van Gaal ameshinda mechi 52 katika michezo 101 aliyowaongoza Mashetani wekundu hao akiwa madarakani.

CHELSEA YAIPIKU MANCHESTER UNITED MAUZO YA JEZI

$
0
0
CHELSEA imeizidi ujanja Manchester United katika mauzo ya jezi miongoni mwa klabu za Ligi Kuu England msimu wa 2015/16, huku ikishika nafasi ya tatu duniani, licha ya kusuasua na kushindwa kjutetea ubingwa.

Mauzo ya jezi za Chelsea yamepanda kwa asilimia 39 kutoka msimu uliopita na kufikia jezi 3,102,000, ikiwa ni asilimia tano zaidi ya mauzo ya United iliyofanikiwa kuuza jezi 2,977,000.

Arsenal imeimarika nafasi ya tatu kwa klabu za England na ya saba duniani ikiuza jezi 2,055,000.

Kwa mujibu wa wakala wa masoko wa vifaa vya michezo, Euroamericas, Barcelona ndio kinara barani Ulaya ikiuza jezi 3,637,000 ikifuatiwa na Bayern Munich iliyouza jezi 3,312,000.

Kuendelea kufanya vizuri kwa Atletico Madrid iliyofanikiwa kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu kumeifanya kuingia 10 bora kwa mara ya kwanza kwa kuuza jezi 1,977,000 idadi ambayo imeiwezesha kushika nafasi ya nane.


Orodha kamili ya vinara wa kuuza jezi ni Barcelona (1), Bayern Munich (2), Chelsea (3), Manchester United (4), Real Madrid (5), PSG (6), Arsenal (7), Atletico Madrid (8), Juventus (9), na AC Milan (10).

PEP GUARDIOLA ATAMBIA UBORA BAYERN MUNICH

$
0
0
KOCHA anayeondoka Bayern Munich, Pep Guardiola, amesema amekuwa kocha bora zaidi katika misimu mitatu ndani ya klabu hiyo, wakati ambapo anajiandaa kucheza mechi yake ya mwisho kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani “Bundesliga”.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona ambaye ameshinda Ligi ya Bundesliga katika miaka yake mitatu, anajiunga na mancheste City ya England msimu ujao.

“Nimejifunza mengi kutoka kwa wachezaji wangu. Ninafurahia uamuzi wangu wa kuja hapa.”

Mechi ya jana kati ya Bayern Munich na Hannover ndiyo iliyokuwa ya mwisho katika katika uwanja wa Allianza Arena kwa Mhispania huyo.


Mechi yake ya mwisho itakuwa ya Kombe la Ujerumani dhidi ya BorussiaDortmund wiki ijayo, huku akitarajia kushinda taji la pili katika kipindi cha miaka mitatu.

AYA 15 ZA SAID MDOE: NANI KAMA MZEE YUSSUF, KHADIJA KOPA NA ISHA MASHAUZI?

$
0
0

Inawezekana kabisa kuwa kuna wasanii wengi wazuri, lakini wenye nyota zao wakawa wachache – hiyo ni tunu ya Mwenyezi mungu.

Lakini pia kunaweza kuwa na wasanii wengi wengi mahiri lakini mwenye mvuto wa kibiashara wakawa wa kutafuta kwa toshi – hili nalo  ndio lile watoto wa mjini wanasema ‘tatizo nyota’.

Naomba niwazungumzie watu watatu wanaokimbiza katika muziki wa taarab – Mzee Yussuf, Khadija Kopa na Isha Mashauzi ambao hakuna ubishi kuwa kwa sasa unapozungumzia biashara ya taarab kwa mlengo wa kimafanikio basi laziwa uvitaje vichwa hivi vitatu kabla hujaendelea kutaja majina mengine.

Kabla ya yote napenda niwaombe radhi wale wote ambao ntakuwa sijawasifu au kuwataja kwenye makala hii maana wakati mwingine huwa inaumiza kidogo pale sifa zilizotukuka zinapokupitia mkono wa kushoto.

Bila kujali mwimbaji au mpiga vyombo, Mzee Yussuf, Khadija Kopa na Isha Mashauzi ndio wasanii wa taarab wenye mashabiki wengi zaidi, ndio ambao kazi zao zinazungumziwa zaidi, ndio ambao uwepo wao kwenye majukwaa ya taarab huteka zaidi hisia za watu.

Jambo hilo si la leo wala jana, ni la zaidi ya juzi. Unawezaje kumkataa Khadija Kopa ambaye amekuwa akitamba miaka na miaka, amekuwa supastaa tangu mwaka 1992 alipotua Dar es Salaam kulitumikia kundi la TOT.

Lakini hata hao TOT hawakumtoa vichochoroni, walimtoa Zanzibar kwenye kundi la Culture akiwa tayari anasumbua kwa kwenda mbele na nyimbo zake kali ukiwemo “Kadandie”.

Tangu kipindi hicho Khadija Kopa hajashuka kisanii wala kibiashara – wako wasanii wengi wa rika lake, aliofanya nao kazi tangu miaka hiyo ya 90 ambao kwa sasa kama hawajafilisika kisanii basi wamefilisika kibiashara au vyote viwili.

Mzee Yussuf, huyu naweza kumwita mwana mageuzi ambaye amekuja kuufanya muziki wa taarab upendwe na kila rika na kila jinsia.

Wala hawajakosea walioamua kumwita Mfalme, hakika Mzee Yussuf ni fundi mwenye sauti ya aina yake, anayejua kulimiki jukwaa, anayejua aina ipi ya tungo itawashika watu. Ubora wa Mzee Yussuf unajitosheleza bila hata kuhangaika kuutaja msururu wa wasanii aliowatoa kisanii.

Kuna mtu mmoja niliwahi kukaa naye jirani katika moja ya maonyesho ya Jahazi wakati Mzee Yussuf akiwa jukwaani akiongea maneno mawili matatu juu ya bendi yake, wala hakuimba siku hiyo. Yule bwana akaniambia kitu flani.

Bwana yule akasema: “pamoja na kwamba leo Mzee Yussuf hajaimba, lakini nimeridhika sana kwa pale nilipomuona tu jukwaani akiongea, nimetosheka na hakika pesa yangu imeenda kihalali, nampenda Mzee Yussuf hata kwa kumuona kwenye matangazo ya biashara ya kwenye TV achilia mbali kumuona akiimba.” Naam hiyo ndiyo ile  nyota ambayo wasanii wengine wengi wanazikosa.

Isha Mashauzi. Mwimbaji mwenye mapafu ya mbwa anayeweza kusimama jukwaani kwa masaa matatu akitupia masauti matamu huku akicheza katika namna ya itakayokufanya usichoke kumtazama.

Aina yake ya kipekee ya uimbaji, inaitoa taarab kutoka kwenye hatua moja hadi nyingine, ni mtu anayebadika kama kinyonga, mtu ambaye akisimama tu jukwaani tayari mashabiki wanapata kiwewe, ubora wake haujalishi nani mtunzi wake, nani anayempigia chombo.

Mzee Yussuf, Khadija Kopa na Isha Mashauzi nawapa pongezi kwa kazi nzuri, kwa kulisongesha gurudumu la taarab, lakini kaeni mkijua kuwa zipo adha nyingi za kuwa juu, zikiwemo kuchukiwa na washindani wenu, kuombewa mabaya na washindani wenu, kufanyiwa majungu na washindani wenu na zingine kadha wa kadha lakini hizo zichukulieni kama moja ya dalili za mtu kuwa STAA, wala hali hiyo isiwasumbue, pigeni kazi. WANAOWACHUKIA NI WACHACHE, WANAOWAPENDA NI WENGI.



CHAZ BABA ASEMA ASHA BARAKA NI MAMA YAKE, TWANGA PEPETA NI NYUMBANI KWAKE

$
0
0

Mwimbaji na rais wa Mashujaa Band Chaz Baba amesema Asha Baraka ni kama mama yake mzazi na hivyo huwa anakerwa sana na wanamuziki wote wanaomtukanaga mmiliki huyo wa Twanga Pepeta.

Chaz Baba aliyasema hayo Jumamosi iliyopita katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni wakati alipotumbuiza na bendi hiyo.

“Mimi bila Asha Baraka nisingekuwa na jina hili nililonalo sasa hivi, Twanga Pepeta na Asha Baraka ndiyo chachu ya umaarufu nilionao katika muziki wa dansi,” alisema Chaz Baba.

“Asha Baraka ni kama mama yangu na Twanga Pepeta ni kama nyumbani kwangu, nawachukia sana wanamuziki wanaomtukana Asha Baraka, huyu ni sawa mama yao” aliongeza mwimbaji huyo aliyewahi kuitumikia Twanga Pepeta kabla hajatimkia Mashujaa Band.

Chaz Baba akafafanua zaidi kauli yake kwa kusema: “Hata majina yao yamefanana. Mama yangu anaitwa Asha Ramadhan na mkurugenzi anaitwa Asha Ramadhan Baraka. Huyu ni mama yangu, nampenda sana.”

Mwimbaji huyo ameyasema hayo katika kipindi hiki ambacho Saluti5 ina nyeti za uhakika kuwa Twanga Pepeta iko mbioni kumalizana na mmoja wa waimbaji wake nyota wa zamani ambaye atatambulishwa kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

ASHA BARAKA NA CHOKORAA KATIKA IJUMAA FLAN TULIVU

$
0
0

Mmiliki wa Twanga Pepeta mamaa Asha Baraka “Mlezi wa wana” hivi karibuni kamera ya Saluti5 ilimkuta akiwa na mwanamuziki wake wa zamani Khalid Chokoraa wakiwa katika hali iliyoonyesha maelewano ya hali ya juu licha ya wawili hao kuwa ni washindani kibiashara.

Chokoraa ambaye ni mmilki wa bendi ya Mapacha Watatu anayomiliki na sambamba na swahiba wake Jose Mara,  ni mmoja wa wasanii waliioondoka Twanga Pepeta kwa mgogoro mkubwa, lakini baadae hali ya hewa ikatulia na sasa kumekuwa na mahusiano mazuri kati ya Twanga Pepeta na Mapacha Watatu.

Wawili hao walipigwa picha hiyo maeneo fulani ya Kinondoni, Ijumaa flani muda mfupi baada ya kutoka msikitini kupata swala ya Ijumaa.

Hata hivyo picha hii haihusiani na tetesi za kati ya Chaz Baba na Chokora mmoja wao kurejea Twanga Pepeta.
 Chokoraa (kushoto) katika kicheko kikubwa wakati akiongea na Asha Baraka
Wakurugenzi wa bendi za dansi Khalid Chokoraa na Asha Baraka

PICHA 10 ZA MAZOEZI MAMESH NA ALL STARS KUELEKEA USIKU WA YA KALE NI DHAHABU

$
0
0

Bendi mbili za zamani Memesh Modern Taarab na All Stars Modern Taraab zipo kwenye mazoezi makali kama sehemu ya maaandalizi ya onyesho kubwa la taarab la “Usiku wa ya Kale ni Dhahabu”.

Onyesho hilo linafanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Dar Live Mbagala ambapo bendi 11 zitajitupa jukwaani kukumbushia ubora wa tungo za zamani.

Nyimbo zinazotarajiwa kurindima Dar Live ni zile zilizotamba kati ya miaka 90 hadi miaka ya mwanzoni mwa 2000.

Mamesh na All Star wameweka kambi yao Magomeni jijini Dar es Salaam katika klabu ya Konga Moyo Band.

Mratibu wa onyesho hilo, Juma Mbizo, ameiambia Saluti5 kuwa bendi zitakazokuwepo Dar Live siku hiyo ya Mei 21 ni Mamesh, All Star, Alwatan, TOT Taarab, Muungano, JKT Taarab, na Babloom Modern Taarab.

Kwa mujibu wa Mbizo Bendi zingine zitakazokuwepo ni Egyption, East African Melody, Zanzibar Stars na Jahazi Modern Taarab.

“Hapo kabla, halijawahi kufanyika onyesho kama hili, hii ni mara ya kwanza katika historia ya muziki wa taraab,” alisema Juma Mbizo.


Pata 10 za mazoezi ya bendi hizo mbili kama zilivyopigwa na Saluti5 leo jioni.
 Bi Mwanaidi Shaaban akifanyia mazoezi nyimbo za Mamesh
Iqujaan Iqbal Hussein akipoza koo na kahawa
Thabit Abdul akipapasa kinanda katika wimbo wa Mamesh
 Mazoezi yakiendelea
 Mbange (kushoto) na Rashid wakipapasa vinanda
 Mmiliki wa iliyokuwa Mamesh Mzee Ahmed (kushoto) akiwa na mratibu wa onyesho Juma Mbizo
 Bi Mwanaidi Shaaban (kushoto) na Mariam Alawi wakiimba wimbo wa All Stars
 Sharif (kushoto) akipiga gitaa la solo sambamba na Thabit Abdul anayekung'uta gitaa la bass
 Walid akiimba wimbo wa All Stars
Mbange akipiga bass gitaa

Viewing all 8805 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>