Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live

LEICESTER CITY NA MTAZAMO WA MSIMU UJAO

$
0
0
KOCHA wa mabingwa wapya wa premier, Claudio Raniel amesema anatarajia ushindani mkubwa msimu ujao kwasababu klabu kubwa zitapania kuhitimisha utawala wao.

Kisha akaweka bayana azma ya kuisuka timu ya ushindani hata katika msimu ujao wa Ligi ya England.

Akinukuliwa, Raniel alisema ubingwa alioupata umewashitua wengi hivyo wanatarajia kupata ushindani mkubwa msimu ujao.

“Hatua ya sisi kutwaa ubingwa imewashitua wengi, hivyo ninachoamua ni kwamba kutakuwa na ushindani mkubwa msimu ujao.”

“Lakini katika mazingira yoyote, tumejifunza jambo muhimu katika Ligi hii na kwamba uzoefu umetupa fundisho kubwa la nini cha kufanya.”

Kikosi cha Leicester kiligharimu pauni milioni 57, kikiwa ndicho cha bei ya chini zaidi miongoni mwa timu zilizopo katika nusu ya kwanza ya jedwali la Ligi hiyo.

“Fedha nyingi hujenga timu kubwa na kama kawaida timu kubwa hushinda, sasa tunaweza kusema ni asilimia 99,” alisema Raniel.

“Msimu ujao itakuwa hali kama hiyo na miaka kumi ama 20 ijayo hali itakuwa kama kawaida, kwamba timu kubwa ndizo zitakazoshindana na sisi hivyo msimu utakuwa mgumu,” alisema meneja wa Leicester.


Raniel alisema kwamba ushindi kama wa timu yake hutokea mara moja katika kipindi cha miaka 20 akitoa mfano wa Nottignham Forest mwaka 1978 na Blackburn Rovers 1995.

MENEJA WA KESSY ACHEKELEA MTEJA WAKE KUTUA YANGA

$
0
0
MENEJA wa beki Hassan Kessy, Athumani Tippo amesema ana furaha kuwa mteja wake ataanza kuitumikia rasmi Yanga msimu ujao baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili utakaoanza mwezi Julai.

Ingawa akadai kuwa ilikuwa ni lazima beki huyo aondoke Simba kwa sababu haikuwa sehemu salama kwake kutokana na jinsi walivyokuwa wakikiuka mkataba.

Tippo alisea kuwa Simba ilifeli kutotimiza vyema yale yaliyokuwa kwenye mkataba wao na Kessy na kwamba walikuwa wakifanya mambo kinyume bila kujali mchezaji huku wakimtuhumu kuwa alikuwa akifanya mambo mabaya.

“Walifeli toka mwanzo, walishindwa wenyewe licha ya kuwa mchezaji alikuwa tayari kuendelea. Kimsingi tumeangalia maendeleo ya mchezaji mwenyewe kwani hata wale waliobaki Simba wakiamua kufunguka maisha magumu wanayoishi unaweza kushangaa.”


“Kessy anaweza kuogopa kuzungumza lakini Simba kuna hali ngumu na ndio maana unaweza kusikia wachezaji wamegoma wakishinikiza kulipwa mishahara huku wengine wakililia stahiki nyingine,” alisema.

ARSENE WENGER AWAPASHA MASHABIKI WA ARSENAL

$
0
0
SIKILIZA kauli ya Arsene Wenger alipowaambia mashabiki wa klabu yake ya Arsenal.

Amewaambia wanazi wa Emirates kuwa, walichokifanya dimbani kwa kumuonyesha mabango ni jambo alilolitarajia na halikumsumbua.

Wenger alikumbana na mabango yaliyomtaka aondoke na kuwaachia Arsenel yao kwa kile walichokidai kuwa wamechoka na kutopata nafasi ya kutwaa ubingwa kwa miaka mingi sasa.

Wenger atatimiza 20 kwenye usukani Arsenal Oktoba, mwaka huu, lakini mara yake ya mwisho kushinda Ligi ilikuwa ni mwaka 2004 na baadhi ya mashabiki waliinua mabango ya kusema: “Wakati wa mabadiliko umefika” uwanjani Emirates.

“Nilidhani uwanja wote ungegeuka na kuwa wa rangi nyeupe kutokana na mabango,” amesema.

“Lengo letu kuu ni kuwafanya watu wote 100% wafurahi. Kwa bahati mbaya hatukuweza kufanya hilo msimu huu.”


Arsenal wanahitaji alama mbili kutoka kwa mechi zao zilizosalia kujihakikishia nafasi katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao, kwa mara 18 mtawalia.

MWIGUKU NCHEMBA MGENI RASMI YANGA IKIKABIDHIWA 'MWARI' WAO

$
0
0

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba Madelu kesho Jumamosi Mei 14, 201 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda na Young Africans katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbali ya Nchemba ambaye atakabidhi Kombe kwa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/16, wageni wengi maalumu watakaokuwa kwenye mchezo huo ni Mkurugenzi wa Vodacom, Ian Ferrao sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi ya Kuu Tanzania Bara (TBLB).

Mchezo huo utafanyika kwa baraka za TPLB baada ya maombi ya Young Africans kukubaliwa na Ndanda ambao watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaoanza saa 10:00 jioni.

Mara baada ya mchezo huo, Mabingwa Young Africans watapewa Kombe la ubingwa, medali na fedha Sh 81,345,723; Mshindi wa Pili Sh 40,672,861; Mshindi wa Tatu Sh 29,052,044 na Mshindi wa Nne atazawadiwa Sh 23,241,635.

Mcehzaji Bora atapewa Sh 5,742,940 sawa na Mfungaji Bora wa Ligi na Kipa bora wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Vodacom, Bia ya Kilimanjaro, Azam, Startimes na NHIF. Mwamuzi Bora atazawadiwa Sh 8,614,610 saw na Kocha Bora wakati timu yenye nidhamu itavuna Sh 17,228,820.

Young Africans ndiyo iliyoomba kwa Ndanda kadhalika TPLB kuomba ridhaa ya mchezo huo kufanyika Dar es Salaam kwa kuwa inatarajiwa kusafiri kwa ndege Jumapili kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidia ya Sagrada Esperanca ya Angola utakaofanyika ama Mei 17 au 18, mwaka huu.

Barua ya Bodi ya Ligi kwa TFF imesema kwamba Young Africans watatumia mchezo huo ambao Ndanda itakuwa mwenyeji kupokea taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara litakalotolewa na Nchemba ambaye mara nyingi anaonekna uwanjani.

Kanuni ya pili ya Ligi Kuu Bara toleo la 2015/16 imeeleza wazi kuwa, “Katika mazingira maalumu, timu inaweza kucheza mchezo wake wa nyumbani katika uwanja mwingine endapo kuna sababu nzito na za msingi, utambulisho wa uwanja katika mazingira haya pia unawajibika kufanywa katika kipindi cha uthibitisho wa kushiriki ligi au kwa maombi maalumu kwa TPLB,” inasema kanuni hiyo.

Kwa kuzingatia kanuni hiyo na sababu za yanga ambazo Ndanda na Bodi wameona kuwa ni nzito wamekubaliana kucheza mchezo huo Dar es Salaam.

Tayari Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameipongeza timu ya soka ya Young Africans kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita wa mwaka 2014/2015.

Hii ni mara ya 26 kwa Young Africans ambayo kwa sasa inacheza mashindano ya kuwania kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kutwaa taji hilo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1965. Simba inafuatia katika rekodi hiyo baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara 18.


“Nichukue nafasi hii kuipongeza Young Africans kwa ubingwa. Pia nizipongeze timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio,” amesema Rais Malinzi baada ya Young Africans kufikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zilizoshiriki ligi hiyo.

JUMA ABDUL AMPONGEZA KESSY KUKUBALI KUTUA YANGA

$
0
0
BEKI wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amempongeza beki Hassan Kessy kwa kukubali kujiunga na Yanga, kisha akadai kuwa; “Njoo tushirikiane ili Yanga iende pazuri kwani tupo sehemu ya mafanikio.”

Beki huyo ambaye amekuwa akifanya vizuri kwa siku za hivi karibuni alisema kuwa anatambua ujio wa Kessy utaleta changamoto kwake na atalazimika kucheza kwa juhudi ili kujihakikishia nafasi.

“Mimi si kocha, anayefahamu atakayecheza ni kocha, lakini nina furaha kuwa Kessy ni sehemu yetu. Najua fika kiwango change kitapanda zaidi na nitaweza kupata fursa kwa kuwa tutakuwa tukishindana.”

“Pia uwepo wake utaisaidia timu na iwapo mmoja wetu hayupo basi mwingine ataweza kuwa na msaada kwenye kikosi. Naamini ni mwanzo lakini kuna mengi ambayo tutaifunza tukiwa pamoja,” alisema Juma.


Kabla ya kusajiliwa Yanga, Juma aliwahi kutamba Mtibwa akiwa ama beki wa kulia na alipotua anga ndipo alipomkabidhi kijiti Kessy ndani ya kikosi cha Mtibwa kabla ya kusajiliwa Simba na sasa Yanga.

ILKAY GUNDOGAN AANGUA KILIO KUKOSA EURO 2016

$
0
0
KIUNGO nyota wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan, amelazimika kuangua kilio kuonyesha namna ambavyo maumivu yanaaribu malengo yake.

Mchezaji huyo atakosa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016), baada ya kuumia goti.

Mjerumani huyo pia alikosa fainali za za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil sababu ambayo ilimfanya kulia kwa uchungu akisema ni kama ana mkosi.

Klabu hiyo ya Bundesliga imesema Gundogan mwenye umri wa miaka 25, aliumia goti wakati anafanya mazoezi na atakuwa nje ya uwanja kwa mechi mbili zilizosaia msimu huu, Fainali za Kombe la Shirikisho la Kandanda la Ujerumani, DFB Pokal dhidi ya Bayern Munich pamoja na Euro 2016.

Habari hizo ni pigo kwa kocha wa Ujerumani, Joachim Loew na pia bahati mbaya mchezaji huyo alikosa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kutokana na maumivu ya mgongo yaliyomweka mkekani kwa miezi 14 kuanzia Agosti, 2013.   
  
Loew amekuwa na matatizo kadhaa ya majeruhi ambapo Bastian Schweinsteiger, Julian Draxler, Emre Can, Jerome Boateng na Benedikt Hoewedes wote wakiwa nje mwaka huu.

Hata hivyo, matatizo hayo yamepungua karibuni ambapo Can, Boateng na Hoewedes wamerejea na kiungo na kiungo wa Wolfsburg Draxler akianza tena mazoezi ya timu yake.

Loew anatarajia kukitaja kikosi cha mwanzo cha Euro 2016 mnamo Mei 17.


Ujerumani itacheza mechi yake ya kwanza ya dimba hilo litakaloandaliwa Ufaransa uni 12 dhidi ya Ukraine mjini Lille na pia itachuana na Ireland ya Kaskazini na Poland katika kundi C.

ARGENTINA YAENDELEA KUTAWALA SOKA LA DUNIA

$
0
0
TIMU ya taifa ya Argentina bado inaongoza orodha ya kila mwezi ya FIFA ya timu bora duniani ambayo imetolewa Ijumaa.

Kwenye orodha hiyo, timu ya taifa ya Ubelgiji ipo kwenye nafasi ya pili ikifuatiwa na Chile.

Ujerumani ni ya tano ikifuatiwa na Hispania na Brazil inachukua nafasi ya saba.

Timu ya bara ya Afrika inayochukua nafasi nzuri kwenye orodha hiyo ya FIFA ni Algeria iliyopo katika nafasi ya 33 ikifuatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 34.

Taifa la Tanzania limeorodheshwa la mwisho Afrika Mashariki katika orodha mpya ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Tanzania imeorodheshwa katika nafasi ya 129 duniani, huku ikishika mkia miongoni mwa mataifa ya Afrika Kusini.


Taifa linaloongoza katika eneo hili la Afrika ni Uganda likiwa katika nafasi ya 72, Rwanda katika nafasi ya 87, Kenya katika nafasi ya 116 na Burundi katika nafasi ya 122.

ZAMOYONI MOGELA AMTAKA MO SIMBA SC… asema Aveva ni bora ajiuzulu tu

$
0
0
GWIJI wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogela amesema kuwa klabu ya Simba inahitaji mabadiliko makubwa kiuongozi ili iweze kwenda na kasi ya mafanikio na Yanga.

Mogela alisema Simba kwa sasa inahitaji mabadiliko kwenye uongozi ili kuwe na utulivu na timu iweze kuendelea.

“Naafiki mabadiliko lakini ambayo yatafuata katiba ya Simba, kama Mohammed Dewji ana nia na ana uwezo wa kuendesha Simba basi apewe ili tupate mabadiliko kwani uongozi wa sasa umeshindwa hata kuwalipa wachezaji kwa wakati.”

“Ninaanza kuamini maneno ya msemaji wa Yanga, Jerry Muro kuwa Simba ni ya matopeni lakini wanaotutia doa ni viongozi na si wachezaji licha ya kuwa walipaswa kucheza kwa mapenzi na kungoja kuliko kufanya mambo kama ya mgomo,” alisema Mogela.


Straika huyo wa zamani aliyetamba kwa jina la “Golden Boy” aliongeza kuwa angependa kuwashauri viongozi kujiuzulu kama wanaona wameshindwa kuliko kuendelea kuhangaika kwani itapelekea wao kutolewa kwa aibu.

PAM D ASEMA AMECHOKA KUSHIRIKISHA WASANII KWENYE NYIMBO ZAKE… adai atasimama mwenyewe ili kujipima kiwango

$
0
0
BAADA ya “kubebwa”, msanii anayekuja kwa kasi katika muziki wa Kizazi Kipya, Pamela Daffa “Pam D”, amesema kuwa sasa umefika wakati wa kusimama mwenyewe ili aone atafika wapi.

Amesema kuwa amesitisha kufanya kazi kwa kushirikisha wasanii wengine akidai kuwa kuendelea kufanya hivyo anaweza kujikuta akilemaa, hivyo ameona akomae mwenyewe.

“Ninajua ninacho kipaji na ninaweza kusimama mwenyewe kama Pam D, hivyo ni wakati wangu sasa wa kutoa ngoma kali lakini siwezi kukataa, Mesen kanipa sapoti kubwa sana mpaka kufika hapa,” amesema Pam D.

Amesema kuwa wakati mwingine akiendelea kushirikisha sana wasanii waliomtangulia, hasa wanaume, anajilemaza na kipaji chake kinaweza kushindwa kuonekana vizuri.

Msanii huyo amesema kuwa kwa sasa anaandaa kibao kipya baada ya kufanya vyema na vibao vyake vya awali vikiwemo “Nimempata” na “Popolipopo”.

ATLETICO MADRID KUVUNA ZAIDI MATANGAZO YA HAKI ZA TELEVISHENI

$
0
0
ATLETICO Madrid itakuwa miongoni mwa klabu zitakazofaidika kwa ukubwa zaidi kwenye dili jipya la uuzaji wa haki za matangazo ya televisheni ya mechi za Ligi Kuu ya Hispania La Liga.

Kwa mujibu wa ripoti inaaminika kwamba Atletico walikuwa wakipata kiasi cha euro milioni 45 mpaka kufikia kiasi cha milioni 100 kwa mwaka.

Los Lojiblancos, mabingwa wa La Liga miaka miwili iliyopita bado wapo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa mara nyingine msimu huu na wamefaidika zaidi kutokana na sheria mpya za mgawanyo wa fedha ambao umetengenezwa ili kuweka usawa kwa kiasi fulani mongoni mwa klabu.

Fedha hizi zitakuza pato mpaka kuzidi mapato ya timu kama mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich ambao wanapokea kiasi cha euro milioni 50 na mabingwa wa Italia, Juventus ambao wnapokea kiasi cha euro milioni 94.

Ni klabu kubwa tu za premier league, mashindano tajiri zaidi duniani, ambao watapokea fedha nyingi zaidi ya Atletico zikiwemo Manchester United, Manchester City na Chelsea ambao watapokea kiasi cha zaidi ya euro milioni 165.


Kanuni mpya ambazo zitaanza kutumika kuanzia msimu ujao zitapunguza nguvu za Madrid na Barcelona ambao wao hupokea kiasi cha euro milioni 140 kila timu na timu nyingine kidogo kama Eibar watakuwa wakipokea kiasi cha euro milioni 43 badala ya euro milioni 18 wakati Sevilla watapokea kiasi cha euro milioni 60.

BASTIAN SCHWEINSTEIGER WA MAN U AGEUKIA FILAMU

$
0
0
MAISHA ni popote, ukona upande mmoja umebana, unageukia upande mwingine ilimradi maisha yasonge mbele.

Ndivyo unavyoweza kusema baada ya nyota mmoja katika kikosi cha Manchester United ambaye anaandamwa na majeruhi, sasa ameamua kuanza maisha mapya wakati akiendelea kujiuguza.

Habari zinasema kwamba nyota huyo Bastian Schweinsteiger anajiandaa kucheza tangazo jipya la iPhone app, Clash of Kings.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani akiwa na kikosi cha Old Trafford ndani ya msimu wake wa kwanza kwenye premier league hajafurahia maisha yake mapya kwenye Ligi hiyo kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwamara huku kukiwa na taarifa huenda akaikosa michuano ya euro 2016 itakayoanza mwezi Juni nchini Ufaransa.

Kiungo huyo mwenye miaka 31, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwamuda mrefu zaidi katika maisha yake ya soka na muda huo atautumia kutengeneza tangazo jipya la Clash of Kings.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild la nchini Ujerumani, Schweinsteiger atacheza kama mfalme kwenye tangazo hilo la kibiashara huku akiwataka watu waunganishe program hiyo ya gemu na kucheza. 

Bado haijawekwa wazi kwamba ni lini tangazo hilo litaachiwa, lakini litakuwa linavutia kumuona Schweinsteiger kwenye sehemu ya tangazo hilo.


Mchezaji huyo ni kama anafuata nyayo za mchezaji wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona kuamua kucheza muvi baada ya kutundika daruga.

ISHA MASHAUZI AIPIGIA DEBE SHOW YA OGOPA KOPA TRAVERTINE

$
0
0

Katika hali iliyoonyesha kuwa hakuna chuki za kibishara kati ya Mashauzi Classic na Ogopa Kopa, mkurugenzi wa Mashauzi Classic Alhamisi usiku aliinadi kwa nguvu show ya Ogopa Kopa itakayofanyika Travertine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi hii.

Akiwa kwenye jukwaa la Mashauzi Classic ndani ya Mango Garden, Isha Mashauzi akawa akilinadi onyesho hilo kila alipopanda kuimba nyimbo zake.

Isha alikuwa akilinadi onyesho hilo pamoja na lile la kwao la kumkaribisha tena kundini mwimbaji Hashim Said ambaye atatambulishwa rasmi Alhamisi ijayo Mango Garden.

“Jumamosi ya ijayo tarehe 14 pale Travertine Hotel Magomeni, kutakuwa na onyesho kubwa chini yake malkia wa mipasho Afrika Mashariki, mama yangu mwenyewe Bi Khadija Kopa katika utambulisho wa bendi mbili – Salam TMK na Ogopa Kopa huku wakisindikizwa na Yamoto Band. Basi unakaribishwa pale kwa kiingilio cha shilingili elfu kumi tu,” alisema Isha kupitia kipaza sauti chake.

MCHEZAJI HUYU WA MAN CITY NAYE PIA AKOSHWA NA KIWANGO CHA MARCUS RASHFORD

$
0
0
Despite only three games remaining this season, the Dutchman has decided to rest Marcus Rashford
KINDA wa Manchester City raia wa Nigeria, Kelechi Iheanacho amekiri kuwa amejifunza mengi kutoka kwa kinda mwenzake wa Manchester United, Marcus Rashford msimu huu na mkutakia mafanikio katika maisha yake ya soka.

Makinda hao mastraika ambao wamekuwa wakilinganishwa uwezo, wameng’ara msimu huu na klabu hizo pinzani za Jiji la Manchester, wakionyesha ubora wa hali ya juu katika kuzifumania nyavu.

Rashford, Muingereza mwenye miaka 18 amepiga mabao saba katika mechi 16 akiwa na United, huku Iheanacho mwenye miaka 19 akifunga 13 katika mechi 34 alizoichezea City.

Iheanacho amevutiwa na Rashford tangu alipoibuka Februari mwaka huu, na amekiri kuwa amejifunza mengi kutoka kwake na anaamini atakuwa mchezaji mkubwa Old Trafford.

"Rashford ni kipaji kichanga cha hali ya juu. Ni “mkubwa”, madhubuti na anafanya maamuzi mazuri, hivyo nadhani anaelekea kuwa mchezaji mzuri wa United miaka ijayo," alisema Iheanacho kuliambia gazeti la Daily Mail.


Akizungumzia kulinganishwa na Rashford, alisema ni changamoto nzuri kwa sababu inampa hamasa na ujasiri zaidi wa kupambana.

CHELSEA BADO YAKOMAA NA JOHN TERRY

$
0
0
Terry is a Chelsea legend - having come through the ranks at the club since he joined aged 14
JOHN TERRY amepewa ofa ya mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea Chelsea msimu ujao wakati akijiandaa kustaafu.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 mkataba wake wa sasa unafikia mwisho kiangazi hiki na alionekana kujiandaa kukosa “sherehe ya kuagwa” Stamford Bridge baada ya kufungiwa mechi mbili kutokana na kulimwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Sunderland wiki iliyopita.

Mashabiki wa Chelsea walikuwa na shauku kubwa ya kumuona mkongwe huyo akibaki Stamford Bridge ili wapate nafasi sahihi ya kumuaga.

Maombi yao yanaonekana kujibiwa, baada ya kocha wao Guus Hiddink kuthibitisha katika mkutano na vyombo vya habari kwamba nahodha huyo amepewa ofa ya kuendelea kucheza kwa mwaka mmoja.

MANCHESTER UNITED YAPIGWA BAO LA KISIGINO NA CHELSEA …Barcelona na Bayern vinara wa kuuza jezi duniani

$
0
0
Manchester United estimate that making do with the Europa League next season will cost them £40million
CHELSEA imeipiga kumbo Manchester United katika mauzo ya jezi miongoni mwa klabu za Premier League msimu wa 2015/16, huku ikishika nafasi ya tatu duniani, licha ya kusuasua na kushindwa kutetea ubingwa.

Mauzo ya jezi za Chelsea yamepanda kwa asilimia 39 kutoka msimu uliopita na kufikia jezi 3,102,000, ikiwa ni asilimia 5 zaidi ya mauzo ya United iliyofanikiwa kuuza jezi 2,977,000. Arsenal inakamata nafasi ya tatu kwa klabu za England na ya saba duniani ikiuza jezi 2,055,000.

Kwa mujibu wa wakala wa masoko ya vifaa vya michezo, Euroamericas, Barcelona ndiyo kinara barani Ulaya ikiuza jezi 3,637,000, ikifuatiwa na Bayern Munich iliyouza jezi 3,312,000.

Kuendelea kufanya vizuri kwa Atletico Madrid iliyofanikiwa kuingia fainali ya Champions League kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu, kumeifanya kuingia kumi bora kwa mara ya kwanza kwa kuuza jezi 1,977,000 idadi ambayo imeiwezesha kushika nafasi ya nane.

VINARA 10 WA KUUZA JEZI 2015/16
1. Barcelona: Mil. 3,637,000
2. Bayern Munich: Mil. 3,312,000
3. Chelsea: Mil. 3,102,000
4. Man Utd: Mil. 2,977,000
5. Real Madrid: Mil. 2,866,000
6. PSG: Mil. 2,212,000
7. Arsenal: Mil. 2,055,000
8. Atletico Madrid: Mil. 1,977,000
9. Juventus: Mil. 1,678,000

10. AC Milan: Mil. 1,287,000

MESUT OZIL KUFANYA KUFURU ARSENAL

$
0
0
Mesut Ozil could become Arsenal's first £200,000-per-week player if he agrees a contract extension

KIUNGO mchezeshaji wa Kijerumani, Mesut Ozil tayari ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Arsenal, lakini mazungumzo ya kusaini mkataba mpya yanakaribia, huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kuongezewa fedha zaidi.

Kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger ameripotiwa kuwa tayari kumfanya Ozil kuwa mchezaji wa kwanza Arsenal kulipwa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.

Ozil amebakisha miaka miwili katika mkataba wake wa sasa unaomuwezesha kulipwa pauni 140,000 kwa wiki, na Wenger ana matumaini kuwa staa huyo atasaini dili jipya kiangazi hiki.

UBINGWA WA LA LIGA NI KUFA NA KUPONA REAL MADRID NA BARCELONA JUMAMOSI HII

$
0
0
Real Madrid's coach Zinedine Zidane waits for the start of a Spanish La Liga soccer match between Real Madrid and Valencia at the Santiago Bernabeu stadium i...
ZINEDINE ZIDANE amewataka vijana wake katika kikosi cha Real Madrid kufunga bao la mapema Jumamosi ili kuipa presha Barcelona katika siku muhimu ya mwisho ya msimu huu wa La Liga.

Real itakutana na Deportivo La Coruna wakati Barca itaifuata Granada.

Ili kushinda taji la La Liga, kikosi cha Zidane kilicho nafasi ya pili na pointi zake 87, kinatakiwa kushinda mechi yake na Barca iliyo kileleni kwa pointi 88 kupoteza.

Pamoja na kwamba taji lipo nje ya mikono ya Real, kocha huyo Mfaransa atajaribu kufanya kila awezalo “kuichanganya” Barca wakati wa mechi.

Ingawa timu hizo mbili zitacheza wakati mmoja katika maeneo tofauti ya Hispania, bila shaka mashabiki wa kila upande watakuwa wakifuatilia mechi ya wapinzani wao, hivyo kupitia kwao habari za kupatikana kwa mabao zitapatikana moja kwa moja kwa makocha na timu zao wakiwa uwanjani.


Deportivo na Granada ziko salama katika mstari wa kutoshuka daraja, hivyo zinatarajiwa kucheza bila presha kwa kuwa hazina cha kupoteza, tofauti na Real na Barca ambazo zinatakiwa “kufanya kweli” kuona nani ataibuka bingwa msimu huu.

MANCHESTER CITY ‘YAANZA’ VIKAO NA N’GOLO WA LEICESTER CITY …Arsenal nayo yakomaa naye

$
0
0
The French midfielder has impressed this season and revealed he will stay with the Premier League winners

MANCHESTER CITY imefanya kikao mara mbili na wawakilishi wa N’Golo Kante kwa ajili ya kumpeleka Etihad kiangazi hiki, ingawa kiungo huyo mapenzi yake ni kuichezea Arsenal au Chelsea, limeripoti gazeti la L’Equipe la Ufaransa.

Staa huyo Mfaransa aliyekuwa na msimu mzuri katika Premier League, kiasi cha kuisaidia Leicester City kushinda ubingwa, amekuwa akihusishwa na uhamisho katika klabu kubwa kuelekea usajili wa kiangazi na kocha ajaye wa City, Pep Guardiola ni shabiki wake mkubwa.

Kwa mujibu wa L’Equipe, habari kwamba Kante anapendelea kucheza London zionzweza kuifurahisha Arsenal ambayo pia tayari imekutana na wawakilishi wa kiungo huyo mwenye miaka 25.

Arsenal inataka kumalizana na Kante kabla ya Euro 2016, ingawa bado haijajulikana kama ndiye lengo lao kuu wakati kukiwa na uvumi kwamba timu hiyo pia inakaribia kumnasa kiungo nyota wa Borussia Monchengladbach ya Ujerumani, Granit Xhaka.

RADJA NAINGGOLAN WA AS ROMA CHELSEA AIKATA MAINI CHELSEA

$
0
0

HARAKATI za Chelsea kutaka kumsajili kiungo nyota wa AS Roma, Radja Nainggolan zinaonekana kugonga mwamba baada ya Mbelgiji huyo kuweka bayana nia yake ya kubaki katika klabu hiyo ya Serie A.

Nainggolan mwenye miaka 28 anatajwa kuwa lengo namba moja la Antonio Conte kiangazi hiki na Chelsea ilishafanya mazungumzo na Roma juu ya uwezekano wa uhamisho wake.

Roma ilikuwa radhi kumwachia kiungo huyo kuondoka kwa “bei ya kueleweka”, lakini mwenyewe amesisitiza kuwa anataka kubaki.

“Nitabaki,” Nainggolan aliwaambia mashabiki wa AS Roma kupitia Sky Italia. “Siondoki hapa. Nina furaha jijini Rome, sitaki kuondoka.”

ZLATAN ABRAMOHIVIC KUONDOKA PSG MAJIRA YA KIANGAZI

$
0
0
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Paris St-Germain, Zlatan Ibrahimovic ameonyesha dalili kwamba ataondoka katika kipindi cha majira ya kiangazi.

Ibrahimovic (34), mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Juzi Ibrahimovic ambaye anatajwa kutakiwa LA Galaxy ya Marekani, ametupia kwenye mtandao wa kija mii akisema:
“Mchezo wangu wa mwisho kesho (leo), huko Parc des Princes. Nilikuja kama mfalme, naondoka kama mkongwe.”

PSG itakuwa wenyeji wa Nantes katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa utakaopigwa leo kabla ya kumaliza mechi za msimu dhidi ya Marseille, Mei 21, mwaka huu.

Muda mfupi baada ya kutupia ujumbe huo, klabu iliweka picha ya mfungaji bora wa msimu ikiambatana na ujumbe “merci Zlatan (asante Zlatan).”

Ibrahimovic ambaye ataiongoza Sweden katika michuano ya Ulaya, alijiunga na PSG akitokea AC Milan mwaka 2012 kwa pauni mil.15.7.

Tangu kutua kwake, amefunga mabao 152 katika mechi 178 alizoichezea PSG. Alikuwa mfungaji bora katika msimu wa 2012/13 na 2013/14.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona ndiye kinara wa upachikaji mabao msimu huu akimzidi Alexandre Lacazette wa Lyon kwa mabao 15 mbele.


Manchester United wamekuwa wakitajwa kumuhitaji Ibrahimovic ambaye ametwaa mataji sita katika klabu tofauti.
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>