Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live

NEW AUDIO: SIKILIZA "WALI NAZI" YA SIKINDE UTUNZI WAKE KARAMA REGESU

$
0
0


Hii ni ngoma mpya ya Mlimani Park Orchestra "Sikinde Ngoma ya Ukae" iliyoachiwa hewani mwishoni mwa mwezi uliopita, utunzi wake mwimbaji aliyerejea kundini Karama Regesu.

Hebu tenga dakika zako kadhaa kusikiliza wimbo huo mtamu.


MAYWEATHER AKIRI KUWA NDIYE CHANZO CHA UVUMI WA KEWAMBA ATAZICHAPA NA CONOR MC GREGOR

$
0
0
FLOYD ‘Money’ Mayweather amedai kwamba yeye ndio chanzo cha uvumi kuwa huenda akazipiga na bingwa mchezo wa mapigano mchanganyiko ‘kick boxing’ na mieleka (UFC), Conor McGregor.

Ripoti zilidai wiki iliyopita kuwa dili limesainiwa kwa Mayweather na MacGregor kuzipiga katika pambano la ndondi litakaloingiza pesa nyingi.

Mayweather ambaye alistaafu mwaka jana, aliiambia tovuti ya fightyhype.com:

“Inawezekana. Inawezekana. Jina hilo la McGregor lilitajwa nami. Uvumi mliousikia ni ambao nimeuanzisha mimi. Unaweza usiwe uvumi.”

McGregor, 27, aliposti picha ya kuunganishwa wakitazamana na Mayweather katika ukurasa wake wa facebook Jumapili na kuchochea uvumi kwamba huenda wawili hao wakapigana hivi karibuni.

Mayweather, 39, aliongeza kwamba anatarajia kuingiza dola mil. 100 kwa yeyote atakayepambana naye.


Kuna uhasama mkubwa baina ya wapiganai hao wawili kwani mara kwa mara wamekuwa wakirushiana maneno kwa miaka mingi.

MKOLONI WA 'WAGOSI WA KAYA' ADAI KUNDI LAO HALIJASAMBARATIKA

$
0
0
FREDRICK Maliki ‘Mkoloni’ ambaye ni mmoja wa kundi la Kizazi Kipya la ‘Wagosi wa Kaya’, amesema kuwa kundi hilo halijasambaratika kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya watu.

Mkoloni amesema kuwa kundi hilo lipo kama kawaida ila limebadili mfumo wa kufanya kazi kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kwavile wasanii wanaounda kundi hilo wanaishi mikoa miwili tofauti.

Kwa mujibu wa Mkoloni, yeye anaishi Dar es Salaam, huku mwenzake, Dk. John Simba akiwa anaishi Tanga, hivyo hata mfumo wao wa kufanya kazi umebadilika.

“Zamani wote tulikuwa tukiishi Tanga ilikuwa rahisi kukutana na kuandaa nyimbo, lakini sasa hadi tupange jinsi ya kuonana ndipo tufanye vitu vyetu,” alisema Mkoloni.


Alisema kuwa anasikitika kusikia watu wakisambaza uzushi kwamba kundi lao limesambaratika na kuundwa lingine linaloitwa ‘The Family’ linalofanya muziki wa Hiphop.

FRANCISCO GENTO ASEMA RONALDO NA BALE WAKISHIRIKIANA WANAWEZA KUFANIKIWA ZAIDI

$
0
0
CHRISTIANO Ronaldo na Gareth Bale ndio wachezaji bora zaidi duniani na kama watashirikiana wanaweza kufanikiwa zaidi, alisema gwiji wa klabu hiyo, Francisco Gento.

Kiwango cha Ronaldo na Bale kimekuwa na mchango mkubwa wa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania pamoja na klabu bingwa Ulaya kwa msimu huu huku Ronaldo akifunga mabao 49 wakati mwenzake akifunga mabao 20.

Hata hivyo, uhusiano wa wawili hao uwanjani umekuwa ukidaiwa ni wa mashaka huku wakisema kuwa wawili hao huwa wanajilazimisha kusema kuwa, wana uhusiano mzuri pale wanapokuwa wakihojiwa na vyombo vya habari.

Gento, ambaye alishinda vikombe sita anatambua uwezo binafsi wa wachezaji hao na anaamini kuwa kama wataunganisha nguvu zao watakuwa hatari zaidi na timu itafanikiwa zaidi.

“Ndio wachezaji bora, ni wachache wa aina hiyo hivyo wakiamua kuungana kwa kufanya kazi kwa ushirikiano watashinda kila taji litakalokuja mbele yao,” Gento alisema.

Madrid inatarajia kucheza mechi yake ya mwisho msimu huu kwa uvaana na Deportivo La Coruna Jumamosi hii na kama watashinda huku Barcelona wakishindwa na Granada ni wazi kuwa watakuwa mabingwa.


Vijana hao wa kocha Zinedine Zidane pia wanatarajiwa kuvaanana wapinzani wao wa jiji la Madrid, Atletico kwenye mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itakayopigwa Mei 28, mwaka huu jijini Milan, Italia.

JUMANNE IDD AJIPA LIKIZO YA MUZIKI NA KUGEUKIA UJASIRIAMALI

$
0
0
MSANII aliyewahi kutamba baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Bongo Star Serch (BSS), Jumanne Idd amesema kuwa sasa ameamua kuweka muziki pembeni na kuelekeza nguvu zake kwingine.

Alisema kuwa, ameamua kufanya hivyo baada ya kuona juhudi anazozifanya ili arejee kwenye gemu bado zinagonga mwamba ndipo akaona ni bora apumzike kwanza.

Amesema kuwa iwapo hapo baadae mambo yatakwenda kulingana na jinsi alivyopanga, basi atarudi kwenye muziki lakini yakiwa kinyume atalazikika kuuweka pembeni.

“Kwa sasa ninafanya biashara zangu Kariakoo Dar es Salaam, ambazo zinanifanya niendelee kuishi mjini, huku nikitafuta nitoke vipi na kama itashindikana sitolazimisha,” alisema.


Amesema kuwa yeye bado ni kijana mdogo ambaye kama Mungu atamjalia kuwa hai anaweza kufanya mambo makubwa hapo baadae, ikiwemo kuingia kwenye siasa. 

JOHN TERRY ABEMBELEZA KUBAKI CHELSEA

$
0
0
JOHN Terry amefichua kuwa angependa kuendelea kukitumikia kikosi cha Chelsea kwa msimu ujao na kuendelea.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 35, Januari mwaka huu alitangaza kuwa ataihama klabu yake hiyo kama itashindwa kumpa ofa ya mkataba mpya.

Ingawa taarifa zilizoenea kuwa Terry alicheza mechi yake ya mwisho kwenye kikosi hicho cha The Blues baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu Jumamosi iliyopita wakati walipopoteza kwa mabao 3 – 2 dhidi ya Sunderland huku akiadhibiwa kukosa mechi mbili zijazo kwenye Ligi.

Hivi sasa nahodha huyo wa Chelsea ameanza kutangaza nia yake ya kuendelea kuwepo Stanford Bridge.

“Bado ninataka kucheza miaka kadhaa mbeleni na matarajio yangu ni kubaki hapa Chelsea,” alisema Terry ambaye ameichezea Chelsea mechi 703 pamoja na kushinda mataji manne ya Ligi Kuu nchini Uingereza.

“Mimi ni mchezaji wa Chelsea nah ii ni klabu yangu tangu nilivyokuwa nina miaka 14, ninaipenda Chelsea.”

Terry alikuwa nchini Denmark Jumatatu iliyopita akiiangalia Brondby IF ambayo inamilikiwa na rafiki yake wa karibu kwa jina la Jan Bech Andersen.

Hata hivyo Terry aliyekuwa akihusishwa na kazi ya ukocha kwenye klabu hiyo ya Brondby, ingawa anatajwa kuwa anaelekea China au Marekani kwa ajili ya kwenda kumalizia kucheza.

Ingawa Terry ambaye alianza kucheza Chelsea aiwa na miaka 21, anahisi kuwa anaweza kupata nafasi ya kuendelea kuwepo kutokana na mahitaji ya kocha mpya wa timu, Antonio Conte ambaye anatarajiwa kuanza kibarua hivi karibuni.


Kocha Guus Hiddink amesema kwamba Terry bado yuko vizuri na anaweza kuendelea kuitumikia Chelea msimu ujao.

BAADA YA RAY, MWASITI ALMASI NAE AJA NA YAKE... asema hivi sasa anavutia kutokana na kula ugali dagaa

$
0
0
MWIMBAJI wa Bongofleva, Mwasiti Almasi amesema kuwa kwa sasa anaonekana anavutia kwasababu anakula vyakula vinavyomfanya awe hivyo tofauti na miaka ya nyuma.

Nyota huyo amevitaja vyakula vinavyomfanya apendeze kuwa ni ugali kwa dagaa pamoja na kujipa muda wa kutosha kupumzika baada ya kupuyanga huku na huko.

“Sio hayo tu, kwa sasa muonekano wangu pia unachangiwa na mahusiano salama ambayo ninayo, ndio maana ninavutia zaidi tofauti na siku za nyuma… nina mapenzi ambayo ni salama,” amesema Mwasiti na kuongeza:

“Siwezi kumtaja kwa sasa kwa sababu bado mapema ila nina faraja sana, ila cha msingi ni kwamba kwa sasa niko kwenye mahusiano ambayo ni salama.”


Mwasiti kwa sasa amekuwa akitamba na ngoma ya “Sema Naye” ambayo amemshirikisha Queen Darleen na amekuwa akiwashauri wasanii wenzake kuwekeza katika muziki badala ya kuridhika na kipato kidogo.

MAJERUHI DANNY WELBECK KUZIKOSA FAINALI ZA EURO 2016

$
0
0
DANNY Welbeck atakosa fainali za Euro 2016 baada ya vipimo vya awali kuonyesha kuwa huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi mitano.

Straika huyo wa Arsenal alipata majeraha ya goti wakati wa ipindi cha kwanza cha mechi yao ya Jumapili waliyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Manchester City baada ya kugongana na Bacary Sagna.

Welbeck alifahamu haraka kwamba tatizo hilo ni kubwa kutokana na uzoefu alioupata katika majeraha mengine tofauti ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja kwa miezi 10.

Vipimo vya awali vimeonyesha kuwa straika hyo, 25, atakosa kuitumikia timu ya taifa ya England katika Euro 2016 na huenda akakosekana pia katika mwanzo wa msimu ujao wa Arsenal.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alifunga magoli matano na kutoa “asisti” mbili wakati waliporejea bada ya kusubiriwa sana Februari na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal Wenger katika siku za mwisho za msimu.


Uthibitisho wa ukubwa wa tatizo ulitarajiwa kutolewa jana, lakini vipimo vya awali vinaonyesha kwamba Welbeck, pamoja na majeruhi Alex Oxlade Chamberlain, hawatashiriki fainali hizo za mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa Juni, mwaka huu.

JONAS MKUDE: SIDHANI KAMA SIMBA ITAMALIZA LIGI HATA KWENYE NAFASI YA PILI

$
0
0
NAHODHA msaidizi wa Simba, Jonas Mkude, amesema hafahamu kama timu yake hiyo itaweza kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu msimu huu, kutokana na jinsi wachezai walivyokata tamaa.

Mkudre amesema hayo baada ya Simba kupoteza mechi dhidi ya Mwadui Jumapili iliyopita, baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Alisema: “Kuna kazi kubwa mbele yetu, nafasi ya kumaliza kwenye nafasi ya pili ipo lakini changamoto ni kuwa wachezaji wengi wamekata tamaa.”

“Hii inatuumiza na mvurugano huu hauwezi kutusaidia kwani kila mchezaji atakuwa akicheza huku akiwa na matatizo.”

“Naamini kama tutatulia tutashinda mechi zetu zilizobaki na tutaweza kumaliza juu ya Azam ambao hadi sasa wana pointi 60, wakiwa wamebakiza mechi mbili wakati sisi tuna pointi 58 uku tukiwa na mechi tatu,” alisema kiungo huyo.

HATIMAYE ROBERTO MARTINEZ ATIMULIWA EVERTON

$
0
0
Roberto Martinez, alone, downcast, arms tightly-crossed, his default position as Everton's season unravelled

ROBERTO MARTINEZ ametupiwa virago na Everton, uamuzi ulioripotiwa kuchukuliwa kufutia timu yake kuchapwa mabao 3-0 na Sunderland Jumatano, matokeo ambayo yamewathibitishia wapinzani wao hao kubaki Premier League.

Everton ambayo kwa sasa inakamata nafasi ya 12 katika ligi, imefanikiwa kushinda mara moja tu katika mechi kumi za mwisho za Premier league.

Kocha huyo Mhispania alitua Goodison Park mwaka 2013, akitokea kufanya kazi Swansea City na Wigan Athletic. Ni kocha wanne kufundisha muda mrefu katika Premier League kati ya makocha wa sasa baada ya Arsene Wenger, Eddie Howe na Mark Hughes.


Martinez mwenye miaka 42, ametimuliwa huku akiwa bado na miaka mitatu katika mkataba wake aliosaini kiangazi cha mwaka 2014.

LUKAKU AJIPIGIA DEBE ASAJILIWE ARSENAL

$
0
0

JORDAN LUKAKU, beki wa kushoto raia wa Ubelgiji ambaye ni mdogo wa straika wa Everton, Romelu Lukaku, amesema hamu yake ni kuichezea Arsenal, na kwamba hatasita kumwaga wino kama klabu hiyo itamfuata kutaka kumsajili.

Staa huyo wa miaka 21 anayeichezea Oostende ya nyumbani kwa Ubelgiji, katika siku za karibuni amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Emirates.

Jordan ni shabiki mkubwa wa Premier League na angelipenda kupata nafasi ya kucheza dhidi ya kaka yake, na amekiri kuwa Arsenal ndiyo timu atakayochagua miongoni mwa nyingine kama zitahitaji huduma yake.


“Premier League ndiyo saizi yangu… Mara zote nimekuwa shabiki wa Arsenal, lakini nina mzuka na kila klabu ya Premier League ili mradi tu isiwe inayopambana kujinusuru kushuka daraja,” alisema.

HASHIM SAID KUTAMBULISHWA RASMI MASHAUZI CLASSIC ALHAMISI IJAYO …mwimbaji mwingine naye yuko njiani kurejea kundini

$
0
0

Baada ya dana dana za hapa na pale, sasa ni imewekwa wazi kuwa mwimbaji Hashim Said amerejea Mashauzi Classic na atatambulishwa rasmi Alhamisi ijayo.

Onyesho hilo la kumkaribisha Hashim Said kwenye bendi yake ya zamani, litafanyika Mango Garden Kinondoni Mei 19.

Hashim anarejea Mashauzi baada ya kujiengua kwenye bendi ya Wakali Wao aliyojiunga nayo mwaka jana.

Mwimbaji huyo ameithibitishia Saluti5 kuwa yeye sasa ni msanii wa Mashauzi Classic na ataanza kazi Alhamisi ijayo katika onyesho litakalojulikana kama “Usiku wa Nyumbani ni Nyumbani”.

Naye meneja wa Mashauzi Classic Sumaragar ameiambia Saluti5 kuwa mbali na Hashim Said, pia siku hiyo kutakuwa na mwimbaji mwingine wa zamani wa Mashauzi Classic atakayerejea kundini.

“Yuko mwimbaji wetu wa kike wa zamani ambaye alibahatika kuimba wimbo mmoja katika moja ya albam zetu, naye anarejea Mashauzi Classic,” alisema Suma na kukataa kutaja jina la mwimbaji huyo.

Aidha, mbali na ujio wa wasanii hao wawili, onyesho hilo litasindikizwa na msanii wa vichekesho Alex wa Machejo (Bingwa wa Rivaz) anayetamba na wimbo wake wa “Ngekewa”.

RAY KIGOSI AWAASA WASANII WENZAKE KUCHAKARIKA WENYEWE BADALA YA KULIALIA KWA VIONGOZI WA SERIKALI

$
0
0
MWIGIZAJI Vicent Kigosi Ray amewakumbusha wenzake kuchakarika na wala wasitegemee mtu wala kiongozi kwamba anaweza kubadilisha maisha yao kama wenyewe hawatakuwa tayari kupambana ili kupiga hatua kwenda mbele.

Msanii huyo amesema kuwa siku zote amekuwa akitamani kuona vijana wenzake wakifanikiwa kwa kupiga hatua kimaendeleo badala ya kubweteka.

“Furaha yangu ni kuona vijawa wenzangu wakifanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo, pambaneni achaneni na mambo yasiyo na msingi, mkitaka kufanikiwa kwenye ndoto zenu fanyeni vitu vigumu,” alisema Ray.

Amesema kuwa wasikae wakategemea kuwa viongozi wa siasa wanaweza kuja kuwabadilishia maisha yao bali jitihada binafsi ndio msingi mkubwa wa mustakabali wamaisha yao.


“Kijana fanya kitu ambacho mwingine hawezi kufanya, hakuna kiongozi yeyote wa nchi atakayekuja kubadilisha maisha yako isipokuwa ni jitihada zako wenyewe huo ndio msingi mkubwa wa mustakabali mkubwa wa maisha yako,” amesema.

JACQUELINE WOLPER ADAI KUACHANA NA MAISHA YA ZAMANI YA "UWALUWALU"

$
0
0
MWIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amesema kuwa ameachana na maisha ya zamani na kuwa mtu mzima ambaye anafanya mambo yake kwa umakini ili kulinda heshima yake mbele ya jamii.

Amesema kuwa, Wolper wa sasa sio yule wa zamani kama ambavyo watu walizoea kumuona na kwamba katika maisha ni muhimu kubadilika kulingana na umri unavyokwenda.

“Nilikuwa ninavaa vile kutokana na wakati ule ulivyokuwa a kuna watu walikuwa wanapenda, lakini hivi sasa nimekuwa mtu mzima na nina mambo yangu binafsi hivyo ni lazima nivae gauni kwani mtu unatakiwa ujibadiliashe wewe mwenyewe usisubiri kubadilishwa,” alisema Wolper.


Wolper amekiambia kipindi cha ‘Nirvana’ kinachoruka kupitia EATV, kuwa ana mchumba ambaye hata hivyo hakumtaja, lakini akaffanua kuwa ni muhimu afanye mambo kulingana na wakati.

THEA WA BONGOMUVI ADAI ANAEPUKA MAJUNGU KWA KUTOJICHANGANYA KWENYE VIJIWE VYA UMBEA

$
0
0
MWIGIZAJI mkongwe wa filamu nchini, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka kuwa hapendi kujichanganya kwenye vijiwe ili kuepuka majungu ambayo yanaweza kumkosanisha na watu wengine.

Amesema kuwa kwa kawaida vijiwe vingi huwa na marafiki na wanafiki na makundi ambayo anaweza kukutana nayo yakamuharibia mipango yake ya maisha.

“Binafsi nimebadili utaratibu wa maisha yangu ili kuepuka marafiki wanafiki niliokuwa nikikutana nao kwenye makundi kama kenye vijiwe vya majungu,” amesema Thea.

Amesema kuwa kwa sasa akitoka kwenye shughuli zake za filamu anarudi zake nyumbani kufanya shughuli nyingine muhimu kwa ajili ya maisha yake na mwanawe.


“Siku hizi nikienda kushuti filamu ninafanya kilichonipeleka kisha ninabadilisha nguo na kurudi nyumbani kwangu, maana sipendi sana kukaa kwenye makundi kwani ndio mwanzo wa maneno maneno na majungu,” amesema.

NDANDA NA YANGA SASA KUCHEZA TAIFA KESHO JUMAMOSI

$
0
0
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Ndanda Fc na Yanga uliokuwa ufanyike uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara sasa utafanyika uwanja wa taifa, Dar es Salaam kesho Jumamosi.

Hiyo inafuatia makubaiano ya timu hizo; Ndanda na Yanga ambayo yamebarikiwana bodi ya Ligi pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga iliipigia magoti Ndanda Fc kuomba mechi ichezwe Dar es Salaam kwasababu wanataka kuwahi Angola Mei, 17 kucheza na wenyeji Sagrada Esperanca katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Ndanda wamekubali kucheza mechi zote mbili za msimu na Yanga ugenini kwasababu hawana cha kupoteza wala kupata zaidi katika Ligi Kuu ilipofikia.


Katika mchezo huo, Yanga itakabidhiwa ombe lake la ubingwa wa Ligi Kuu iliyojihakikishia Jumapili baada ya Simba SC kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC uwanja wa Taifa, Dar es Salam.

RAPHAEL VARADE WA REAL MADRID ANUKIA MANCHESTER UNITED

$
0
0
TAARIFA za tetesi za usajili za mwishoni mwa juma lililopita zinamtaja nyota wa Real Madrid, Raphael Varane kuwa ana asilimia kubwa ya kutua katika kikosi cha Mashetani Wekundu wa Old Traford.

Ukubwa wa tetesi hizi zinafuatia ukweli mwingine pia, Varane ana mahusiano ya karibu na anayetajwa kuwa atakuja kuinoa Manchester United, Jose Mourinho.

Imefahamika kuwa Mourinho amemweka katika orodha ya usajili wake pindi akichukua jukumu la kukinoa kikosi cha United.

Daily Star limemwelezea Varane kama ni mchezaji wa awali aliye katika malengo ya Mourinho na kwamba wawili hao wameshaanzxa kuteta.

Hata hivyo, United wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vigogo wengine wa soka barani Ulaya ambao nao wameweka nia ya kumsainisha beki huyo.

Mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich, Liverpool, Juventus na Paris Saint-Germain wamo katika mbio za kuwania saini ya Raphael Varane.

Varane amekuwa akikosa namba ya kudumu katika kikosi cha Los Blancos cha msimu huu baada ya kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane kuwapa nafasi kubwa walinzi Sergio Rams na Pepe.

Varane mwenye umri wa miaka 23, ameelezwa kutoficha mapenzi aliyonayo kwa kocha Jose Mourinho tangu akiinoa Chelsea.

Hata alivyokuwa ndani ya Real, Mourinho alikuwa akimwamini Varane kiasi cha kupangwa mara kwa mara tofauti na sasa ambapo amekuwa akipangwa kwa nadra na Zidane.


Hata hivyo, akinukuliwa na Sky Sports kuhusiana na uvumi huu, kocha Zidane alisema, inawezekana kuna timu zinamuhitaji Varane, ikiwemo Manchester United, lakini taarifa za klabu yake hazina mpango wa kumruhusu aondoke.

CANNAVARO: AZAM WASAHAU KUSHINDA KOMBE LA SHIRIKISHO LA TFF

$
0
0
NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub “Cannavaro” ametamka wazi kuwa Azam wasahau kushinda Kombe la Shirikisho la TFF na badala yake wamepanga kutwaa Kombe hilo pamoja na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Cannavaro alisema: “Hakuna cha kushindikana, tuna uwezo wa kutwaa Kombe lolote lile tunaloshiriki. Kinachotakiwa ni malengo pekee na kuchukulia kila mchezo kama mchezo wa fainali.”

“Kwanza Azam wasahau kutushinda kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho, pia tupo kwenye michuano ya Kimataifa si kama wasindikizaji, tumekuja kupambana na hicho ndicho tunachotufanya.”

“Naamini hakuna kitakachoshindikana sisi kama Yanga tutafanya mambo ambayo hayakushuhudiwa na naamini tunaweza kutwaa Kombe hilo la pili kwa ubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu,” alisema.

Nahodha huyo pia alisema kuwa licha ya kwamba wametangazwa ni mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu huku kukiwa na michezo miwili haijachezwa, anaamini kuwa watashinda mechi zote zilizobaki.


Yanga tayari imefikisha pointi ambazo haziwezi kufikiwa na klabu nyingine ya Ligi lakini itaendelea na michezo mingine miwili baada ya Ligi kumalizika Mei 21, mwaka huu.

BAFETIMBI GOMIS WA SWANSEA ATENGEWA PAUNI MILIONI 18 PSG

$
0
0
PARIS Saint-Germain sasa ipo tayari kuweka mezani kitita cha pauni 18milioni kwa ajili ya kumnasa straika wa Swansea, Bafetimbi Gomis, hii ni kwa mujibu wa Sky Sports.

Straika huyo raia wa Ufaransa ameingia katika rada za PSG inayotaka kuendeleza ubabe katika Ligi ya Italia.

Dalili za Bafetimbi kutua katika kikosi cha mabingwa watetezi zinatiwa nguvu na taarifa za kwamba kiwango chake kwa sasa kimewavutia baadhi ya mawakala wa klabu mbalimbali.

Tayari PSG wameteta na wakala wa nyota huyo na kwamba hata Swansea wenyewe wamethibitisha taarifa za kuweko kwa pirika kuhusiana na straika huyo.

Wakitambua hilo, PSG wamemtengea kiungo huyo kitita cha pauni 18 milioni wakiongeza dau waliloliweka awali ambalo lilikuwa pauni 15 milioni.

PSG walimthaminisha Mfaransa kuwa ni wad au la 18 milioni, ingawa wameonyesha dalili za kukubali kushusha kiwango.

Swansea pamoja na kuweka bayana thamani ya mchezaji huyo, wamethibitisha kuwa straika huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na klabu mbalimbali za Ulaya.

“Bafetimbi anawindwa na timu nyingi za Ulaya, lakini nataka acheze katika kikosi ambacho atapata namba ya kudumu.”


“Mchezaji mwenye ofa nyingi, ila ni jambo la kusubiri kuona ifikapo kipindi cha usajili kikifika mwisho.”

ABDALLAH KIBADENI ATAMBA KUICHAKAZA SIMBA SC

$
0
0
KOCHA wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni amesema kuwa anaamini kikosi chake kitashinda mechi mbili za mwisho kwenye Ligi ili kujihakikishia wanamaliza na pointi 35.

JKT Ruvu inatarajia kuvaana na Mgambo mwishoni mwa wiki, kabla ya kucheza mchezo wake wa mwisho msimu huu kwa kuvaana na Simba kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Kibadeni alisema, “Ni lazima nipate pointi sita ndiyo nitakuwa salama. Pointi tatu si salama kwetu kabisa. Namini kwa jinsi wachezaji wa Simba walivyo kwa sasa, tutaweza kuwafunga na tutawashangaza.”

“Mwadui, Toto zilipata matokeo dhidi ya Simba, kwanini sisi tushindwe? Tuna kila sababu ya kufanya vyema kwenye mechi yetu ya mwisho,” alisema kocha huyo.


Kibadeni alichukua mikoba ya kuinoa JKT Ruvu ikiwa kwenye hali mbaya baada ya kuongozwa kwenye mechi nane za Ligi na kocha Fred Minziro ambaye kwa sasa anaifundisha Panone FC ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>