Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

MANCHESTER UNITED YAREJEA ANGA ZA 4-0 … Valencia, Mkhitaryan, Lukaku, Martial wainyamazisha Everton

$
0
0

Manchester United imeikung’uta Everton 4-0 kwenye mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Antonio Valencia alifunga bao linalostahili kuingia kwenye mabao bora ya msimu kwa shuti kali la dakika ya nne.

Matic alitoa pasi ndefu ya juu kutoka upande wa kushoto iliyoenda kwa Valencia upande wa kulia ambapo beki huyo akiwa nje ya 18 akaungaunisha kwa mkwaju mkali uliomshinda kipa Jordan Pickford.

Kipindi cha pili ndicho kilichokuwa na heka heka zaidi kwa pande zote, lakini ni Manchester United iliyofanikiwa kupata magoli mengine matatu katika dakika kumi za mwisho wa mchezo.


Henrik Mkhitaryan aliyepewa pande tamu na Lukaku alifunga bao la pili dakika ya 83 huku Lukaku naye akitupia wavuni goli la tatu dakika ya 89 kabla Anthony Martial hajafunga la nne dakika ya 90 kwa njia ya penalti.

Nahodha wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney aliyejiunga na Everton, alishindwa kufurukuta na alipumzishwa dakika ya 82.

Hii ni mara ya tatu msimu huu kwa Manchester United kushinda 4-0 kwenye Premier League.

MAN UTD (4-3-3): de Gea, Valencia, Bailly, Jones, Young, Fellaini, Matic, Mata (Herreraat 77), Mkhitaryan (Martial 88), Rashford (Lingard 60), Lukaku 

EVERTON (3-4-3): Pickford, Keane, Jagielka, Williams, Martina, Schneiderlin, Gueye (Calvert-Lewin 76), Baines, Davies (Sandro 66), Sigurdsson, Rooney (Mirallas 81)



Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>