MTAYARISHAJI na mtunzi wa muziki, Pharrell Williams ametimiza miaka 44 ya kuzaliwa kwake lakini muonekano wake ni kama kijana wa miaka 18!
Staa huyo amesema kuwa anatumia maji kwa wingi na kufanya mazoezi sana kabla ya kazi za muziki.
Pharrell aliongeza kwamba yete sio muumin wa unywaji pombe uliopitiliza hivyo kuchangia kuwa na mwenokano wa ujana.
“Watu wanaweza kushangaa kwanini naonekana kujana, lakini siri kubwa imejificha kwenye ufanyaji mazoezi na ratiba ya unywaji maji,” alisema staa huyo.