WINGA mkongwe, Frank Ribery amesema kwamba hakuwa kwenye mpango wa kutaka kutua nchini England katika dirisha lililopita.
Ribery amesema kuwa taarifa zilizokuwa zikimuhusisha kutaka kumalizia soka lake nchini England hazikuwa na ukweli wowote.
Ribery alikuwa akihusishwa kutaka kuhamia katika klabu ya Manchester City ya nchini England, jambo ambalo amedai ulikuwa ni uvumi tu.