Mshambuliaji kinda wa Manchester United Marcus Rashford amesema kuumia kwa Paul Pogba ni pengo kubwa lakini anaamini ukubwa wa kikosi cha Muorinho utasaidia kupunguza makali ya pengo hilo.
Pogba ameumia msuli wa paja na atakuwa nje ya dimba kwa muda usiopungua wiki nne.
"Tutapwaya kumkosa Pogba, natumai atarejea mapema uwanjani," alisema Rashford na kuongeza: "Tunafarijika kuwa na kikosi kipana na hili ndiyo jambo jema kwa kocha na kwa wachezaji kwa ujumla kwasababu siku zote tunapigania nafasi ya kucheza."