Habari hizi si njema kwa Manchester United. Kiungo Paul Pogba atakuwa nje ya dimba kwa mwezi mzimma baada kuumia kuumia misuli ya paja wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Basel Jumanne usiku.
Mfaransa huyo wa miaka 24 alifanyiwa uchunguzi kuhusu jeraha hilo Jumatano na ikabainika kwamba Pogba atakosa kucheza angalau kwa mwezi mmoja ingawa kuna uwezekano pia kuwa akakaa kwa wiki mbili zaidi ya muda uliokadiriwa.
Pogba huenda akaukosa mchezo wa Premier League dhidi ya Liverpool 14 Oktoba ingawa kocha Jose Mourinho anaamini kiungo wake anaweza akawa fiti kushiriki mchezo huo.
Mechi atakazokosa Pogba ni dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace, pamoja na mechi ya Kombe la Ligi raundi ya tatu Jumatano dhidi ya Burton.
Kadhalika, ataikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya CSKA Moscow mnamo 27 Septemba.
Aidha, atakosa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema mwezi Oktoba.