KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola ameripotiwa kuonyesha kusikitishwa kwake na kitendo cha kumkosa beki Jonny Evans.
Manchester City ilikuwa ikimwania beki huyo kwa nguvu lakini klabu ya West Brom ikataja dau kubwa.
Hata hivyo, klabu hiyo inaweza kufufua mpango huo katika dirisha la Januari, mwakani.