KOCHA wa timu ya Mbao FC, Etienne Ndayiragije amesema kuwa sababu ya kuanza kwa kusuasua kwa kikosi chake ni uwepo wa namba kubwa ya wachezaji vijana ambao hawana uzoefu na michuano ya Ligi.
Kocha huyo alishuhudia kikosi chake kikifungwa dhidi ya Singida United hadi kuambulia kipigo cha 2-1 Dodoma Mbao FC ya Mwanza imepoteza mechi ya Jumapili, Septemba 10, 2017 ilipocheza dhidi ya Singida United kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mbao imefungwa 2-1 na kupoteza pointi tatu, mechi yao ya ufunguzi wa Ligi walishinda ugenini dhidi ya Kagera Sugar.
“Tuna wakati mgumu kidogo kwasababu wachezaji wengi ni vijana ambao hawana uzoefu na mechi za Ligi Kuu bara, tunahitaji kukaa pamoja kwa kipindi kirefu zaidi,” alisema kocha huyo.
Mbao msimu uliopita walikuwa moto baada ya kufika fainali katika michuano ya Kombe la FA dhidi ya Simba, ingawa walipoteza mchezo huo.