Paul Pogba huenda akakosekana uwanjani kwa wiki tatu au zaidi baada ya kupata maumivu ya misuli ya paja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Basle.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 alitolewa dakika ya 19 baada kuumia kwenye harakati za kugombea mpira.