Nemanja Matic anaamini Manchester United inahitaji kushinda mechi kama za Stoke City iwapo inahitaji kutwaa taji la Premier League.
Kikosi cha Jose Mourinho kilianza msimu kwa kishindo na kushinda mechi zote tatu za mwanzo lakini ikawa na wakati mgumu pale iliposafiri kwenda bet365 Stadium, Jumamosi na kuambulia sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City.
"Ulikuwa mchezo mgumu," kiungo huyo mkabaji aliiambia MUTV. "Siku Stoke City imekuwa ngumu kwenye uwanja wake wa nyumbani. Ni timu ngumu ili tulazimu kuambulia pointi moja.