Nahodha wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney akiwa na kikosi cha Everton, atarejea Old Trafford Jumapili ya Septemba 17 kukabiliana na timu yake hiyo ya zamani.
Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Rooney dhidi ya Manchester United tangu alipoihama na kurejea klabu yake ya utotoni.
Rooney mwenye umri wa miaka 31 atacheza mchezo huo huko kesi yake kuendesha gari akiwa amelewa ikisikilizwa siku moja baadae, Septemba 18.
Kocha wa Everton Ronald Koeman amesema amesikitishwa sana na mashtaka ya kuendesha gari akiwa mlevi ambayo yanamkabili mchezaji wake Wayne Rooney ambaye aliachiwa huru kwa dhamana.
Rooney alikamatwa muda mfupi baada ya saa nne usiku saa za Uingereza usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya polisi wa Cheshire kusimamisha gari lake aina ya VW Beetle eneo la Wilmslow.