MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard maarufu kama “Ben Pol” ameamua kuachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo “The Best of Ben Pol” itakayoanza kuwa mtaani Ijumaa hii.
Mkali huyo wa RnB Septemba 8 atasheherekea siku yake ya kuzaliwa huku akichia albamu hiyo, ambayo itakuwa ikimfikisha miaka 8 katika muziki wa kizazi.
Akizungumzia ujio wa albamu hiyo pamoja na wimbo wake mpya unaoitwa “Kidume” ambao amemshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Chidinma, Ben Pol akasema kuwa uamuzi wake wa kutoa albamu ni kutaka kuendelea kuwa karibu na mashabiki wake.
Ben Pol alisema ametoa albamu hiyo yenye mchanganyiko wa nyimbo zake mbalimbali mpya na za zamani huku akiamini kuwa itakuwa ni zawadi nzuri kwa mashabiki wake na kwa mashabiki wa muziki kwa ujumla.
Alisema kuwa katika albamu hiyo kuna nyimbo kama “Kidume”, “Tatu” na “Tuliza Boli”, “Nikikupata”,“Maneno”,“Jikubali”, “Yatakwisha” , “Sophia”, “Moyo Mashine”, “Pete” na “Phone”.