Miamba ya muziki wa dansi The African Stars “Twanga Pepeta” ni miongoni mwa burudani kubwa zitakazopatikana Dar Live Mbagala Jumamosi hii katika tamasha la Fulldozi lililoandaliwa na ITV, Radio One na Capital Radio.
Twanga Pepeta imepata bahati ya kuwa bendi pekee (kwa dansi na taarab) kushiriki onyesho hilo kubwa litakalopambwa na wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya.
Burudani nyingine zitakazopatikana Dar Live Jumamosi hii ni pamoja na show kutoka kwa Snura na mkali wa masauti Beka Flavour anayetesa na ngoma zake kali “Libebe” na “Sikinai”.
Aidha, katika Fulldozi Concert pia atakuwepo Q Chillah, Sholo Mwamba, Juma Nature na wengine kibao.