Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

OKWI, KASEJA MBIONI KUREJEA SIMBA SC... wamo pia mastaa wengine watatu kutoka timu nyingine

$
0
0
SIMBA imesikia kwamba baaadhi ya timu zimeanza kuwinda majina ya wachezaji wake kuelekea usajili ujao wa Ligi Kuu msimu wa 2017/18 lakini haijali.

Badala yake wekundu hao wa Msimbazi tayari wamejibu mapigo kwa staili yake baada ya kuwapa mikataba ya awali wachezaji watatu matata waliofanya vyema kwenye Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara msimu huu.

Saluti5 inajua kwamba mastaa hao watatu ambao tunalazimika kuhifadhi majina yao kwa sasa tayari wana uhakika mkubwa wa kuichezea Simba na mazungumzo yao na yamefikia patamu hivi sasa.

Katika uchunguzi wetu tumegundua kwamba wachezaji hao walikuwa jijini Dar es Salaam wikiendi hii na wameshamalizana na mratibu anayeendesha mpango huo.

Wachezaji wanaotajwa kwamba wanaweza kusajiliwa Simba ni pamoja na Emanuel Okwi ambaye ni Mganda anayerejea Msimbazi kwa mara nyingine, kiungo wa Mbeya City, Kennny Ally pamoja na mshambuliaji wa Kagera Sugar ambaye anacheza kwa mkopo kwenye timu hiyo akitokea Simba Mbaraka Yusuf Abeid.

Lakini pia Simba wanadaiwa kufanya mipango ya kumrejesha kipa wake wa zamani, Juma Kaseja ambaye naye yuko Kagera Sugar na amekuwa katika kiwango kikubwa sana.


Hata hivyo habari zinasema kwamba mastaa watatu waliochinjwa jijini Dar es Salaam toka juzi sio hao wanaotajwa mara kwa mara.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>