KOCHA mkuu wa timu ya mpira wa wavu Magereza ya jijini Dar es Salaam, Edwin Masinga amepania kuibuka na ubingwa wa mashindano ya kuwania Klabu Bingwa ya Muungano.
Mashindano hayo yanaendelea kutimua vumbi katika uwanja wa ndani wa Dar es Salaam ambapo vikosi vya Magereza wanaume na wanawake ni miongoni mwa timu zinanoshiriki.
Pamoja na Magereza timu nyingine zinazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Jeshi la Polisi Zanzibar, Moro Stars, Kinyerenzi, Sekondari ya Makongo, Mjimwema, saut Mwanza, Tanga na Dodoma.
Akizungumza na saluti5, Masinga alisema ameviandaa vikosi vyake kama hatua ya kutaka kutimiza azma yao ya kuibuka na ubingwa wa mashindano hayo yanayoshirikisha timu kutoka Tanzasnia Bara na visiwani.
Alisema kutokana na hilo, anaamini ubingwa utakwenda kwa timu za wanaume na wanawake wa timu za Magereza ikifika mwishoni mwa michuano hiyo itakayofikia tamati April 26, mwaka huu.
Alisema kuwa pamoja na kwamba katika mchezo kuna matokeo ya kushinda au kushinda, hata hivyo timu zake zimejipanga kuhakikisha zinapata matokeo mazuri katika mchezo yote ambayo itawakabili na hatimaye kufikia fainali kuibuka na ubinga.