Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

REAL MADRID, BARCELONA WAPIGANA VIKUMBO KUMWANIA VICTOR LINDELOF

$
0
0
KLABU mahasimu katika La Liga, Real Madrid na Barcelona zimeingia katika vita vya usajili wa msimu ujao na kujikuta wakimwania kwa pamoja Victor Lindelof.

Pamoja na vigogo hao wa Ligi ya Hispania, pia Manchester United wanatajwa katika mbio hizo za kumwania nyota huyo wa klabu ya Benfica.

Mlinzi huyo kijana amekuwa katika kiwango bora katika msimu huu kiasi cha kuzigonganisha timu mbalimbali, lakini Sky Sports imezitaja Barca na Real Madrid kuwa ndizo zilizoonyesha nguvu kubwa kupata saini yake.

Lindelof mwenye umri wa miaka 21, yumo pia katika kikosi cha timu ya taifa ya Sweden, alikuwa katika orodha ya wachezaji wanaoweza kuuzwa, lakini tarifa za hivi karibuni zimesema kuwa, Benfica imesitisha azma hiyo.

Imebainika kuwa, Benfica imesitisha nia ya kumweka sokoni beki huyo baada ya kuondokewa na mlinzi wao mahiri, Renato Sanches aliyejiunga na Bayern.

Katika kuhakikisha haimpotezi Lindelof, imeamua kuweka mezani ofa kubwa ya euro mil 40 ambapo imebainika klabu za Barca na Madrid wanaweza wasipande dau hilo.


Wakati ambapo Real Madrid wakishikilia msimamo wa kutaka kumng’oa beki huyo kwa upande wa Barcelona tayari wameripotiwa kumwania mlinzi atakayeziba nafasi ya Marc Bartra.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>