Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

COUTINHO ASEMA JURGEN KLOPP NDIYO MPANGO MZIMA LIVERPOOL

$
0
0
Jurgen Klopp reportedly lifted his players spirits with a rousing speech at the end of season party
MAJOGOO wa Jiji, Liverpool bado hawajarejea katika mstari wa mafanikio tangu kuanza kwa msimu huu, lakini straika Philippe Coutinho amemfagilia kocha wake, Jurgen Klopp kwa kusema ameweza kuleta mabadiliko yanayoonyesha matumaini makubwa.

Coutinho mwenye umri wa miaka 23, amenukuliwa akisema kuhusu Klopp kuwa tangu achukue jukumu la kuinoa Liverpool amefanya timu kurudi taratibu katika mstari japo kuna changamoto nyingi za kukaa kileleni.

“Ukiniuliza mimi ninaweza kukuambia jambo moja kuwa Klopp ni kocha bora kwa sababu ameibadili timu tangu pale alipopewa jukumu.”

“Liverpool ya sasa ni tofauti na ile iliyokuwa chini ya Brendan Rodgers, kuna tofauti kubwa hata ya namna timu inavyocheza kwa wachezaji kushirikiana dimbani.”

“Tangu atue Anfield mwezi Oktoba, mwaka jana ameonyesha mambo mapya ambayo sisi kama wachezaji tunaweza tukawa sehemu ya kuzungumzia mabadiliko haya,” alisisitiza mwanandinga huyo raia wa Brazil.

“Tunacheza tukiwa na furaha na imani kubwa chini ya Klopp, kama atapewa muda zaidi wa kuwa hapa nina imani kuna jambo linaweza kubadilika na hata timu kurejea katika kiwango cha soka zamani.”

“Tupo katika mwendo wa mafanikio, tunarudi katika mstari wetu wa siku nyingi nyuma ambapo soka letu lilikuwa katika kiwango chetu cha kawaida.”

“Ni kipindi ambacho hata mashabiki wetu ni lazima watambue kuwa tunapita katika kipindi cha mpito, lakini katika kipindi kifupi baadae Liverpool itabadilika na kuwa timu ya ushindani kama zamani.”

“Tukiwa mazoezini utaona namna tunavyowajibika huku tukifurahia mbinu zake mpya ambazo zinatufanya tuwe katika kiwango bora. Klopp ni kocha anayeangalia mbele kwa mtazamo wa mafanikio ya baadae,” alisisitiza Coutinho.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>