Mwimbaji wa dansi mwenye hits kibao Christian Bella amerejea nchini baada ya mapumziko yake ya takriban miezi minne huko Sweden.
Hata hivyo Bella hajaja mikono mitupu bali ameshuka na mpango wa kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la “Nishike”.
Mwimbaji huyo aliyerejea Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, tayari ameshaingia studio chini ya producer Abby Daddy kama wanavyoonekana pichani juu kwaajili ya wimbo huo mpya.
Bella anatarajiwa kufanya onyesho kubwa kabla ya mapumziko ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo ngoma hiyo mpya nayo itatambulishwa.