MWANAMUZIKI Ommy Dimpoz amesema kuwa, sasa ana uhakika hatasumbuliwa tena na vimwana ambao wamekuwa wakimganda kumtaka kimapenzi kwakuwa tayari ameshamuweka wazi mpenzi wake.
Amesema kuwa katika maisha yake huwa hapendi kuweka wazi mambo ya mahusiano ya kimapenzi, lakini amelazimika kumuonyesha mpenzi wake ili kuepuka usumbufu ambao amekuwa akiupata mara kwa mara.
“Huo ndio ulikuwa msimamo wangu, lakini sasa nimelazimika kuuvunja kwa nia nzuri tu ya kuondoa usumbufu huu wa kufuatwa kila mara na wasichana wanaonitaka kimapenzi,” amesema Dimpoz.
Amesema kuwa wapo wasanii ambao wamekuwa wakipenda kuiga utamaduni wa kigeni kwa kuweka mambo yao ya mahusiano ya mapenzi kwenye mitandao ya kijamii, jambo abalo kwake hakulifikiria.
“Yaani imenibidi tu nifanye hivyo, laini kwa kweli si kawaida yangu kuweka wazi mambo binafsi yakiwemo ya mapenzi, ila nimewaonyesha mchumba wangu ambaye anasoma ng’ambo, nina uhakika sitasumbuliwa tena,” alisema.