MWANAMUZIKI Najma Dattan ambaye ni mchumba wa Baraka da Prince amewataka wale wanaowafuatilia na kuwachunguza waache kufanya hivyo kwa vile wameamua wenyewe kuwa wachumba.
Kimwana huyo amesema kuwa tangu apelekwe kwa kina Baraka jijini Mwanza, wapo watu ambao wamekuwa wakizusha maneno kwamba yeye (Najma) ameshawahi kutembea na mastaa mbalimbali.
“Niwaambie tu kwamba hilo kwetu halina nafasi kwa sababu hawajui tumefanya nini hadi tukaamua kuwa pamoja, hivyo ninawaambia wanapoteza muda wao bure kutufatilia,” amesema Najma.
Amesema kuwa wawili wanapokubaliana katika mambo ya maisha huwa wamepitia njia nyingi ambazo wanaamua kuzisahau na kuanza moja na kwamba anashangaa kuona baadhi ya watu wakiushikia bango uchumba wao ambao hauwahusu.
“Kama hawaelewi, basi waendelee kusema, mimi sijali kwamba Baraka ametoka na wangapi wala yeye hawezi kujali kwamba nimetoka na wangapi kwasababu hayo ni maisha ya nyuma ambayo tumeshayaacha,” amesema.
Najma amekuwa akihusishwa na Mr. Blue na Diamond Platinumz zamani.