Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

JUVENTUS WAWANIA SAINI YA SAMIR NASRI

$
0
0
KIBIBI kizee cha Tulin, Juventus wanajiandaa kutuma ofa ya pauni 23 milioni wakitaka saini ya straika wa Manchester City, Samir Nasri.

Tarifa za ndani ya klabu ya Juve zinasema kuwa, Nasri amewekwa katika orodha ya wanandinga wanaowaniwa na vinara hao wa Seria A.

Awali, Juventus walimweka katika orodha ya usajili wa majira ya kiangazi mwaka jana lakini taarifa za sasa zinasema kuwa wanambakiza straika huyo katika usajili wa kiangazi.

Lakini hatua ya Juve inaweza kudunda kwa sababu bosi wa matajiri wa jiji la Manchester, Manuel Pellegrini amekana kila hatua ya kuondoka kwa mchezaji yeyote katika kikosi chake.

Akinukuliwa, Pellegrini alisema klabu yake haina mpango wa kuuza mchezaji katika kipindi cha uhamisho cha majira ya kiangazi.

Kocha huyo ambaye yupo katika siku za mwisho za kuhudumu kama bosi wa timu hiyo, ameziambia timu zinazowania saini ya Nasri kuwa hauzwi hata kwa dau nono.

“Sitotaka kuona ninamwacha mchezaji muhimu katika kipindi hiki cha usajili wa mwezi Januari, badala yake ninajipanga kwa ajili ya kiangazi.”


“Ninajipangakwa ajili ya kufanya usajili mkubwa wa majira ya kiangazi na hiyo ndio tageti yangu na ninasimama katika ukweli huo,” alisema Pellegrini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 8805

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>