
MANCHESTER UNITED imeripotiwa kutenga pauni milioni 30 kwa ajili ya ofa ya uhamisho wa kiungo nyota wa Leicester City, N’Golo Kante.
Kante amekuwa na mchango mkubwa kwa Leicester msimu huu, na tayari amehusishwa na kuhamia katika klabu kadhaa kubwa barani Ulaya kiangazi hiki.
Gazeti la Star limedai kuwa United inajiandaa kuwa ya klabu ya kwanza kupeleka ofa rasmi Leicester kwa ajili ya kiungo huyo wa miaka 25.
Awali iliripotiwa kuwa United iko tayari kumtoa kwa mkopo kinda wake Mbrazil, Andreas Pereira kama sehemu ya dili hilo.