Hatimaye waimbaji Zubeda Mlamali na Aisha Vuvuzela wametambulishwa rasmi Jahazi Modern Taarab katika onyesho kubwa lililofanyika Travertine Hotel usiku wa kuamkia leo.
Umati mkubwa ukafurika Travertine kuwapokea wasanii hao wapya waliojiunga na Jahazi kiasi cha wiki tatu zilizopita.
Pamoja na kwamba wasanii hao hawakupata fursa ya kutambulisha nyimbo zao mpya kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali, lakini walikonga nyoyo za mashabiki wao kwa kupiga nyimbo maarufu za bendi hiyo zilizoimbwa na wasanii wengine.
Zubeda akatesa na nyimbo za Khadija Yussuf huku Vuvuzela akikamua nyimbo za Fatma Shobo.
Ilikuwa ni bonge la shangwe ambalo lilikolezwa pia na waimbaji wengine kama Fatma Mcharuko, Mishi Mohamed na Fatma Kassim ambao nao walitesa kinoma huku Mfalme Mzee Yussuf naye akiwatia wazimu washabiki wake nyimbo zake kali zilizokolezwa na vionjo vipya kabisa.
Aisha Vuzuzela amejiunga na Jahazi akitokea Wakali Wao Modern Taradance wakati Zubeda Mlamali ametokea East African Melody.
Mbali na waimbaji hao mpiga bass Rajab Kondo aliyejiunga na bendi hiyo tangu mwishoni mwa mwaka jana, naye alitambulishwa rasmi. Kabla ya kutua Jahazi, Rajab Kondo alikuwa akiitumikia Mashauzi Classic.
Aisha Vuvuzela jukwaani
Aisha Vuvuzela akimwanga minenguo
Sehemu ya umati uliokuwa ukicheza nyimbo za Jahazi
Kulikuwa na 'surprise' ya keki ya siku ya kuzaliwa ya Fatma Kassim ambapo pichani anaonekana akimlisha keki ndugu yake Shinuna Kassim
Fatma Mcharuko alifanya vema sana
Fatma Kassim akienda kumpa bakshishi Fatma Mcharuko
Mkurugenzi msaidizi wa Jahazi Khamis Boha akila keki ya birthday ya Fatma Kassim
Zubeda Mlamali (kushoto) akijiachia na Fatma Mcharuko jukwaani
Mzee Yussuf akiimba wimbo "Wasiwasi wako"
Nyumbani ni nyumbani, Mussa Mipango naye alikuwepo
Mzee Yussuf akikamua na madansa wake
Rajab Kondo (kushoto) akitambulisha na Prince Amigo
Huyu ni shabiki maarufu anayekwenda kwa jina la Fataki. hapo akijiachia na shabiki wa kike
Tashwira ya Travertine ilivyokuwa
Hapa Vuvuzela (kulia) akijiachia na Fatma Kassim
Zubeida Mlamali kwenye jukwaa la Jahazi usiku wa kuamkia leo