WIMBO mpya wa TOT Plus Band “Wivu" utunzi wake Abdul Misambano (pichani), umetinga kwenye Top Ten ya kipindi cha Afro Dance cha radio TK FM ya Tanga.
TK FM (Tanga Kunani) kwa sasa ndiyo radio yenye mashabiki wengi zaidi katika mji wa Tanga huku moja ya vipindi vyake bomba ni Afro Dance inayopiga nyimbo za dansi za Tanzania na kwingineko barani Afrika.
Wimbo “Jiamini” ambao ni project binafsi ya Isha Mashauzi umeendelea kushika namba moja kwa wiki ya tatu mfululizo.
Chati hizo huwekwa hadharani kila siku za Ijumaa kupitia kipindi hicho cha Afro Dance kinachoruka kila siki (kasoro Jumamosi) kuanzia saa saa 2.10 usiku hadi saa 4 usiku chini ya mtangazaji Roger Kiss.
Itazame chati ya Top Ten ya Afro Dance ya TK FM ujionee nani kapanda nani kashuka. USIKILIZE PIA HAPO JUU KABISA WIMBO “JIAMINI” ULISHIKA NAMBA 1
Chati ya Top Ten ya Afro Dance ya TK FM