Quantcast
Channel: saluti5
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live

MARIAH CAREY AMKIMBIA MPENZI WAKE

$
0
0


MWANAMUZIKI maarufu duniani, Mariah Carey, amehama kutoka kwenye jumba la kifahari la mpenzi wake, bilionea James Packer.
Watu wa karibu wa mkongwe huyo wanasema kuwa, Mariah alihma pamoja na wasaidizi na wafanyakazi wake wote na kuliacha tupu jumba hilo lililoko Beverly Hills Mansion, jijini Los angelos.
Akizungumzia hilo, Mariah alikiri kuhama lakini hakubainisha sababu na pia hakutaka kusema amehamia wapi.

Z ANTO AOTA KUREJEA KWENYE CHATI

$
0
0


MSANII Z Anto amesema kuwa wimbo mmoja tu unaweza kurudisha heshima yake kama atazingatia vitu vinavyohitajika kwenye muziki.
Akiongea na Saluti5 z Anto alisema kuwa bado ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa kuwa anaamini hakuna kitu kikubwa kilichobadilika.
“siku zote huwa naamini kurudi kwa msanii wa aina yoyote huwa kunakuja kwa kazi moja peke yake, kwa hiyo suala la kurudi katika hatua ambayo niliiacha, sio kazi kubwa kihivyo, kwasababu ubora wa kazi moja peke yake unaweza kunirudisha kwenye makali yangu,” alisema.
Alisema, akiwa na usimamizi mzuri na ngoma anayoikusudia kuitoa, itaweza kumrudisha huku akidai kuwa na kazi nzuri pekee haitoshi, inatakiwa kuwa na usimamizi mzuri wenye uwezo wa kumsimamia vema katika kazi zake.

NI ALHAMISI YA KIHISTORIA … MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAM YA “SURA SURAMBI” NOVEMBA 26 MANGO GARDEN …East African Melody, Cassim Mganga ndani ya nyumba

$
0
0

Hatimaye albam ya “Sura Surambi” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab, inazinduliwa Alhamisi hii Novemba 26.

Albam hiyo kutoka kwao Mashauzi Classic, itazinduliwa ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni huku kundi kongwe la taarab East African Melody, likizindikiza tukio hilo kubwa.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa albam ya “Sura Surambi” inaundwa na nyimbo sita kali.

Ni Alhamisi ya kihistoria ambayo Isha anaitaja kuwa itapambwa na ratiba iliyokwenda shule itakayomwacha mshabiki apate uhondo mwanzo mwisho.

Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na “Sura Surambi” aliouimba yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji wake Abdumalick Shaaban, na “Mjinga Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.

Nyimbo nyingine alizozitaja Isha ni “Pendo la Ukakasi” wa Saida Ramadhan, “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga na “Mapenzi Yamenivuruga” mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed. Nyimbo zote hizo sita zimetungwa na Isha Mashauzi.

Mbali na Melody, mkali wa tungo za mapenzi wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga naye pia atasindikiza uzinduzi huo wa “Sura Surambi” ndani ya Mango Garden Alhamisi hii.

AZAM FC KUINGIA KAMBINI WIKI HII TAYARI LIGI KUU

$
0
0

TIMU ya Azam FC inaanza kambi rasmi wiki hii kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania, katika mchezo dhidi ya Simba utakaochezwa Desemba 12, mwaka huu.

Kwa sasa, wachezaji ambao hawako katika kikosi cha taifa, wapo mapumzikoni wakisubiri wenzao wamalizane na jukumu hilo wajiunge pamoja kwa maandalizi ya mchezo huo.

akizungumza na Saluti5, msemaji wa Azam, Jaffar Idd alisema maandalizi yataendelea kwa baadhi ya wachezaji kwani wengi wapo kwenye timu zao za taifa zinazoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji.

“Timu yetu inaingia kambini wiki hii na kikubwa tunafikiria mchezo wetu ujao dhidi ya Simba, lengo ni kuhakikisha tunafanya vizuri na kuendelea kuwa vinara wa Ligi,” Alisema.

Azam inaongoza Ligi ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mchezo wa tisa, kushinda minane, kupata sare moja na ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja.

ARSENE WENGER BADO ANAPIGA HESABU ZA KUBORESHA KIKOSI CHAKE

$
0
0

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba bado anajaribu kuangalia kikosi chake kabla hajaamua kusajili mchezaji yoyote dirisha dogo.

Wenger alisema kwamba ameanza kazi hiyo ili kuangalia uwezekano wa kujaza baadhi ya nafasi katika timu hiyo.

Alisema hiyo imetokana na kuwepo wachezaji kadhaa majeruhi, huku wengine uwezo wao ukiwa umeshuka.

"Naangalia uwezo wao, nidhamu yao pamoja na mambo mengine, pia wapo baadhi ya wachezaji wanataka kuondoka hivyo lazima nafasi zao nizijaze," alisema.

VAN GAAL SASA AWEKA MATUMAINI KIBAO KWA MEMPHIS DEPAY

$
0
0

BILA hiyana, kocha wa klabu ya Manchester United, Louis Van Gaal, ameweka wazi kuwa hivi sasa wanasafiria nyota ya shujaa wao mpya, Memphis Depay.

Van Gaal amesema, Manchester United ambayo kwa sasa inapambana kurejea katika ubora wake, inaamini winga huyo raia wa Uholanzi mwenye miaka 21, atatimiza matarajio yao.

Memphis aliyejiunga na United msimu huu akitokea PSV Eindhoven ya Uholanzi na kupewa jezi namba saba, ambayo ilikuwa ikitumiwa na mastaa waliong’ara ndani ya klabu hiyo, amethibitisha kuwa atalinda heshima ya namba hiyo.

mchezaji huyo mwenye kasi na chenga za maudhi, aliyezaliwa Februari 13, 1994 mjini Moordrecht, Uholanzi, aliigharimu United paundi mil.31.

Winga huyo aliyechezea PSV Eindhoven mechi 90 na kuifungia mabao 31 kwa miaka minne aliyodumu hapo ameonyesha matumaini makubwa Old Trafford.

Alitua United kiangazi cha mwaka huu na wengi wa mashabiki walidhani kocha Van Gaal amembeba kwasababu ni Mholanzi mwenzake.

“Kwa hakika, Depay ameonyesha uwezo mkubwa licha ya kwamba bado hana uzoefu wa kutosha, lakini ameonyesha ni mchezaji wa aina gani na sasa klabu imeweka matarajio kwake,” alisema Van Gaal.

Alisema, mchezaji huyo aliyebadilishwa kutoka mchezaji wa benchi na kuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha PSV, analizoea soka la Uingereza kwa haraka.

Mbali ya Van Gaal, mshambuliaji mahiri wa zamani wa zamani wa Liverpool, Dirk Kuyt, ameifagilia klabu hiyo akisema imelamba dume kwa kumsajili Memphis.

“Kwa muda mfupi niliofanyakazi na Memphis kwenye timu ya taifa ya Uholanzi, nimejiridhisha kuwa ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na atakuwa staa baadae,” alisema.

Amesema mchezaji huyo amekuwa hajivungi kujifunza kutoka kwa magwiji na makocha, jambo litakalomfanya kukamilika kiuchezaji.

NEYMAR HASOMEKI BARCELONA ...MAN CITY NA MAN UNITED ZATAJWA KUMVURUGA AKILI

$
0
0

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona FC, Neymar hasomeki kabisa kwenye suala linaloitwa msimamo na sasa inadaiwa amepanga kuondoka katika timu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na gazeti moja la nchini Hispania, imeeleza kuwa nyota huyo amepanga kuondoka baada ya kutokuwa na  namba ya kudumu hususan kwenye eneo la ushambuliaji wa kati.

Tayari kuna taarifa kuwa, huenda akatua ndani ya kikosi cha timu ya Manchester City kwa ajili ya kuichezea msimu ujuo huku Manchester United nayo pia ikihusishwa katika kukivuruga kichwa cha mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil.


JOSE MOURINHO AWATAKA MASHABIKI WA CHELSEA WASAHAU KUHUSU UBINGWA WA PREMIER LEAGUE

$
0
0

KOCHA mkuu wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekiri wazi kuwa atakuwa anadanganya kama wafanyavyo wasanii wa maigizo ikiwa atasema kikosi chake kitaibuka na ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Hata hivyo Mourinho amesema licha ya kupoteza imani ya kutetea taji, lakini bado hajakata tamaa ya kumaliza mbio za ubingwa huo akiwa ‘top four’.

Kauli ya kocha huyo inakuja baada ya mwishoni mwa wiki timu yake kuichapa Norwich bao 1-0 kupitia kwa straika Diego Costa ambapo Mourinho alikataa kuwa ushindi huo ndio mwanzo wa kutetea ubingwa wa Premier League.

“Kumaliza katika nafasi nne za juu ni jambo linalowezekana kwangu. Utakaponiuliza kuhusu kuchukua ubingwa nitakwambia kuwa haiwezekani, labda Tom Cruise (mwigizaji wa Marekani) anaweza kufanikisha hilo. Nafasi ya nne ni ngumu kuipata lakini inawezekana," alisema Mourinho.

"Ushindi huu unatia moyo. Tulikuwa na presha. Tulihisi hilo lakini tuliendana na hali hiyo na tukafanikiwa kupata matokeo tuliyoyahitaji sana,” aliongeza kocha huyo mwenye maneno mengi.

LIONEL MESSI FULL KICHEKO KUREJEA DIMBANI ...asema mapambano yanaendelea

$
0
0

STRAIKA Lionel Messi amejivunia kurejea uwanjani wakati wa mchezo ambao timu yake ya Barcelona iliweza kuondoka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid wikiendi iliyopita.

Staa huyo wa timu ya taifa ya Argentina amekuwa nje ya uwanja tangu mwishoni mwa Septemba, lakini Jumamosi akaingia akitokea benchi kipindi cha pili cha mchezo huo wa Classico uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu.

"Ushindi huu mnono kwenye El Classico na kurejea kwangu uwanjani ni mambo ambayo yananifanya nijisikie vizuri licha ya kuwa bado nina safari ndefu, tutaendelea kupigana kushinda kila mechi tutakayocheza,” alisema nyota huyo.


Ushindi huo umefanya ishuhudiwe Barcelona ikiwa mbele kwa pointi sita dhidi ya vijana hao wa Rafael Benitez kwenye kilele cha msimamo wa Ligi hiyo ya La Liga.

ARSENAL YAFUFUA MATUMAINI ULAYA , YASHINDA 3-0 …Bayern Munich nayo yalamba mtu 4-0

$
0
0

Arsenal imefufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Champions League baada ya kuinyuka Dinamo Zagreb 3-0.

Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 6 na itahitaji kushinda mchezo wake wa mwisho Disemba 9 dhidi ya Olympiakos ili kusonga mbele.

Bayern Munich imejihakikishia kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuitandika  Olympiakos 4-0.

Mabao ya Arsenal inayoshikilia nafasi ya tatu nyuma ya Bayern Munich na Olympiakos, yalifungwa na Mesut Ozil na Alexis Sanchez aliyetupia mipira wavuni mara mbili.

Kwa upande wa Bayern Munich wauaji walikuwa ni Douglas Costa, Robert Lewandowski, Thomas Muller na Kingsley Coman.

Huu ni msimamo wa kundi F huku kila timu ikiwa imebakiza mchezo mmoja.

CHELSEA YACHARUKA IKUA 4-0 LIGI YA MABINGWA, PORTO YASHIKWA PABAYA ...kundi lao bado halitabiriki

$
0
0
Chelsea playmaker Oscar celebrates with the ball under his shirt as he looks to the sky in celebration of his 77th minute goal
Mabao yaliyofungwa na Gary Cahill, Willian, Oscar na Kurt Zouma yameipa Chelsea pointi tatu muhimu kufuatia ushindi wake wa 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv katika mchezo wa kundi wa Ligi ya Mabingwa.

Wakati Chelsea ikiua 4-0, Porto iliyokuwa inaongoza kundi G, imeshushwa hadi nafasi ya pili baada ya kufungwa 2-0 na Dynamo Kyiv.

Porto na Chelsea zote zina pointi 10, lakini mabingwa hao wa England wanaogoza kundi G kwa wastani mzuri wa magoli.

Dynamo Kyiv ni tatu kwa pointi zake 8 na kufanya nafasi ya kufuzu kwenda 16 bora iwe wazi kwa timu zote tatu za juu kutegemea na matokeo yao ya mwisho yatakavyokuwa Disemba 9 ambapo Chelsea itaumana na Porto na huku Maccabi Tel Aviv wakiwa uso kwa uso na Dynamo Kyiv.

Msimamo wa kundi G huu hapa.

MESSI MWAMCHE TU, AIONGOZA BARCELONA KUIFUMUA ROMA 6-1 ...BATE Borisov na Bayer Leverkusen zatoshana nguvu

$
0
0
Lionel Messi amedhihirisha kuwa majereha yaliyomweka nje ya dimba kwa wiki kadhaa, hayajapunguza makali yake.

Mshambuliaji huyo ameng’ara sana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma ambapo timu yake ya Barcelona imevuna ushindi wa bao 6-1.

Kama vile hiyo haitoshi, Messi akafunga mara mbili huku Luis Surez nae akifunga mara mbili wakati Gerard Pique na Adriano wakifunga mara moja kila mmoja.

Bao pekee la Roma lilifungwa na Eden Dzeko dakika ya 90, dakika nane baada ya mshambuliaji huyo kupoteza mkwaju wa penalti.

Huo ulikuwa mchezo wa kundi E ambao ulishuhudia pia timu za BATE Borisov na Bayer Leverkusen zikitoshana nguvu kwa sare ya 1-1. Barcelona tayari imefuzu kwenda hatua ya 16 bora.
Lionel Messi made it 2-0 when the Argentine put the finishing touch to a sensational 29-pass move on Tuesday nightLionel Messi akifunga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa
Messi lifts the ball over the advancing Roma goalkeeper Wojciech Szczesny to score second goal at the Nou CampMessi akifanya vitu vyake Nou Camp
Barcelona ace Messi took just 18 minutes to get on the scoresheet on his return to action after two months out with an injury Messi alipofunga bao la kwanza dakika ya 18 
Msimamo wa kundi E


MASHAUZI CLASSIC YAWEKA HADHARANI RATIBA YAKE YA UZINDUZI WA “SURA SURAMBI” ALHAMISI HII MANGO GARDEN

$
0
0

Mashauzi Classic Modern Taarab wameweka wazi ratiba yao ya uzinduzi wa albam yao ya “Sura Surambi”.

Albam ya “Sura Surambi” yenye nyimbo sita kali, inazinduliwa Alhamisi hii ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.

Akiongea na kituo cha radio cha Magic FM Jumapili mchana, mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi akasema watakaofungua pazia la burudani ni East African Melody kuanzia saa 3.30 usiku hadi 6 za usiku, baada ya hapo kutakuwa na nusu saa itakayoshuhudia burudani ya Cassim Mganga pamoja na nasaha fupi.

Isha Mashauzi akafafanua kuwa Mashauzi Classic watapanda jukwaani saa 6.30 usiku na kumimina burudani mfululizo hadi mwisho wa onyesho.

Saluti5 pia ilifanikiwa kuongea na Isha Mashauzi ambapo alisema nyimbo zote sita za albam mpya zitapigwa live kabla ya mashabiki kupewa bonasi ya wimbo mpya kabisa utakaopatikana albam ijayo.

Wimbo huo ni “Kismet” kutoka kwake mwenyewe Isha Mashauzi.

Isha pia amesema mashabiki watakaokwenda Mango Garden watapata wasaa wa kupiga picha kwenye red carpet kabla ya kujitosa ukumbini.

ZENIT ST PETERSBURG YAITUNGUA VALENCIA 2-0 NA KUWEKA HISTORIA YA AINA YAKE CHAMPIONS LEAGUE ...Lyon yakalishwa 2-1 na KAA Gent

$
0
0
Zenit St Petersburg imejihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi H katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Valencia 2-0 huo ukiwa ni ushindi wao wa tano mfululizo.

Oleg Shatov aliwafungia wenyeji bao la kwanza dakika ya 15 kabla ya  Artem Dzyuba kuihakikishia ushindi Zenit kwa bao la dakika ya 74. 

Ukiwa umesalia mchezo mmoja kwa kila timu, Zenit inajihakikishia kumaliza ya kwanza ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo katika historia yake ya   Champions League hatua ya makundi.

Katika mchezo mwingine wa kundi H Lyon ilikubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa KAA Gent.
Artem Dzyuba (right) celebrates with Danny (left) after scoring in his side's 2-0 win over Valencia 
Artem Dzyuba (kulia) akishangilia na Danny(kushoto)  wa Zenit  baada ya kufunga kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Valencia 
Zenit and Valencia were playing in frosty conditions, with a snowman near the pitch showing how cold it was
Zenit na Valencia walicheza kwenye umande mkubwa huku barafu likitanda kando ya dimba 
Zenit inaongoza Kundi H ikiwa imeshinda mechi zake zote tano ilizocheza katika hatua ya makundi  Champions League 

WAYNE ROONEY NA ANTHONY MARTIAL WAREJEA KUIKABILI PSV EINDHOVEN

$
0
0

Wayne Rooney na Anthony Martial wamerejea mazoezini Manchester United  tayari kwa kuikabili PSV Eindhoven katika mechi ya Champions League Jumatano usiku.

Washambuliaji hao tegemezi walikosa mchezo wa Premier League Jumamosi iliyopita dhidi ya Watford kutokana na maumivu ya miguu lakini wote waliripoti mazoezini Jumanne asubuhi.
The Manchester United players looked relaxed, despite the arctic conditions, as they prepare for the Champions League clash Wachezaji wa Manchester United wakifanya mazoezi Jumanne asubuhi
Red Devils boss Louis van Gaal (right) chatted with his captain  at the Aon Training Complex as they walked out to the pitches
 Louis van Gaal (kulia) akizungumza na Rooney


PICHA 12: ISHA MASHAUZI AKIWA STUDIO KUREKODI KIGONGO KIPYA “KISMET”

$
0
0

Isha Mashauzi “Queen of the Best Melodies” au malkia wa masauti ukipenda, ameingia studio kurekodi wimbo wake mpya kabisa unaokwenda kwa jina la “Kismet”.

Isha akiwa na kundi zima la Mashauzi Classic, amerekodi wimbo huo katika studio za Sofia Records chini ya producer Ababuu Mwana Zanzibar.

Huo ni wimbo utakaopatikana katika albam ijayo ya Mashauzi Classic Modern Taarab, ukiachana na “Sura Surambi” inayozinduliwa Alhamisi hii Mango Garden Kinondoni.

“Hakuna kulala, mwisho albam moja ndiyo mwanzo wa albam ijayo”, alisema Isha Mashauzi katika maongezi yake na Saluti5.

“Huu ni utaratibu wangu wa siku zote, kuisindikiza albam inayozinduliwa kwa kigongo kitachopatikana albam ijayo,” anafafanua Isha.

“Kismet” ni utunzi wake Isha Mashauzi ambapo ndani ya wimbo huo, mwimbaji huyo anasema anawawakilisha wale wote ambao wako ndani dimbwi la mapenzi yaliyokolea raha, mapenzi yasiyo na kokoro wala chembe ya maudhi.

Isha ameiambia Saluti5 kuwa “Kismet”  ambayo tayari inatingisha kwenye kumbi za burudani wanazopiga Mashauzi Classic, inaingia hewani wiki hii.
Isha Mashauzi akirekodi wimbo wake mpya  wa taarab uitwao "Kismet"
 Isha Mashauzi akivuta hisia 
 Asia Mzinga akijiandaa kutia masauti kwenye wimbo "Kismet" wa Isha Mashauzi
Producer Ababuu akiwa mtamboni 
Kalikiti Moto kwenye kinanda
Rajab Kondo akilingurumisha gitaa la bass wakati wa kurekodi wimbo mpya wa Isha "Kismet"
 Isha Mashauzi ametupia masauti ya hatari sana kwenye "Kismet" ni balaa
  Sijui ni hisia au ndo kamkumbuka happiness wake!
Hizo ndo raha za "Kismet" huyu ni mwimbaji Naima Mohamed akishiriki kurekodi wimbo wa Isha
 Isha Mashauzi ndani ya Sofia Records
Anaitwa Pishuu Meshaa akikung'uta solo gitaa kwenye "Kismet"
Zubeida Malick nae akiweka sauti kwenye"Kismet"
Hivi ndivyo 'cover' ya promosheni ya wimbo mpya wa Isha Mashauzi uitwao "Kismet" inavyoonekana





KOCHA BARCELONA ASEMA MESSI BADO ANAHITAJI UANGALIZI

$
0
0
Messi returned to the starting line-up with a two-goal performance against the Italians in Group E
KOCHA wa Barcelona, Luis Enrique, amesema kwamba staa wake Lionel Messi bado anahitaji muda ili kurejea kwenye kiwango chake, baada ya kupona majeraha ya goti. 

“Nadhani anaonekana kuwa vizuri, nafurahi pamoja na mashabiki wote wa Barca pamoja na klabu kuona akirejea uwanjani na kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa,” kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari.

Amekuwa kifanya mazoezi ya kucheza, lakini anachotakiwa ni kupewa muda ili aweze kujenga mguu na kuchaji betri zake na baada ya hapo tutamfurahia tena Messi,” aliongeza kocha huyo. 

ZIDANE ASEMA KWA SASA HANA NJOZI YA KUFUNDISHA REAL MADRID

$
0
0
Zinedine Zidane has revealed that he is not looking to replace Rafa Benitez in charge of Real Madrid this term
NYOTA wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Zinedine Zidane, amesema huu sio muda sahihi wa yeye kuifundisha klabu yake hiyo ya zamani.

Baada ya Madrid kupokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya watani wao Barcelona kwenye mchezo wa El Clasico ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, kuna habari zinasema kuwa, kocha wa klabu hiyo, Rafael Benitez ana uwezekano wa kufukuzwa kazi.

Kutokana na hali hiyo, Zidane ambaye anaifundisha timu B ya klabu hiyo (Castilla), ameonekana kuwa miongoni mwa makocha ambao wanafikiriwa kuchukua nafasi ya Benitez, lakini mwenyewe amesema kuwa hayupo tayari kwa sasa.

“Kwa sasa mimi ni kocha wa Castilla na Benitez ni kocha wa kikosi cha kwanza, najisikia kuwa na amani katika nafasi niliyonayo.


“Ni mapema mno kusema naweza kuwa kocha wa kikosi cha kwanza, huu sio muda sahihi kwangu kufundisha timu hiyo, bado nitaendelea kuwa katika kikosi hiki na kikosi cha kwanza atakuwa Benitez,” alisema Zidane. 

HATIMAYE SIKU IMEWADIA, MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAM MPYA LEO USIKU MANGO GARDEN

$
0
0

Leo usiku ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni kutakuwa na tukio kubwa la kiburudani ambapo Mashauzi Classic Modern Taarab, watazindua albam yao mpya ya “Sura Surambi”.

Uzinduzi wa albam hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, utasindikizwa na kundi kongwe la taarab - East African Melody.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameiambia JAMBO LEO kuwa albam ya “Sura Surambi” inaundwa na nyimbo sita kali.

Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na “Sura Surambi” aliouimba yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji wake Abdumalick Shaaban, na “Mjinga Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.

Nyimbo nyingine alizozitaja Isha ni “Pendo la Ukakasi” wa Saida Ramadhan, “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga na “Mapenzi Yamenivuruga” mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed. Nyimbo zote hizo sita zimetungwa na Isha Mashauzi.

Mbali na East African Melody, mkali wa tungo za mahaba Cassim Mganga naye pia atasindikiza uzinduzi huo wa albam ya “Sura Surambi”.

WENGER ALIA NA UEFA KUHUSU MATOKEO YA ARSENAL NA DINAMO ZAGREB

$
0
0
Arsene Wenger's Arsenal have their fate back in their own hands
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amelitupia lawama Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA), kwa kuruhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu baada ya kushindwa kuiadhibu Dinamo Zagreb kwa kumchezesha mchezaji ambaye anatumia dawa hizo wakati timu hizo zilipokutana mwezi uliopita.

Katika mchezo huo wa Kundi F uliopigwa Septemba 16, ambao Dinamo iliichapa Arsenal mabao 2-1, mchezaji Arijan Ademi alicheza dakika zote 90 lakini baadae alipopimwa alibainika kuwa na matumizi ya dawa hizo.

Baada ya kubainika, UEFA ilimfungia Ademi miaka minne, lakini matokeo ya mechi hiyo yameendelea kubaki hivyohivyo, kitu ambacho anakilalamikia Wenger.

“Ndio na inanishangaza kuhusu uamuzi huu. UEFA imekuwa ikitumia sheria ambazo wameziandaa lakini wamekuwa hawazitekelezi kutokana na kwamba kama kuna mchezaji amebainika kutumia dawa, lazima na matokeo yabatilishwe, lakini kama hawakufanya hivyo wanakuwa wamekubaliana na matumizi ya dawa hizo,” alisema Wenger.

Alisema, kama Shirikisho hilo linakubaliana na hali hiyo, hawana jinsi bali watalazimika kuangalia kiwango chao.  
Viewing all 8805 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>