Mshambuliaji nyota wa Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu hadi nne baada ya kuumia kwenye mchezo wa sare ya 0-0 dhidi ya Chelsea Jumapili mchana.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema: "Danny amefanyiwa vipimo leo, hatujui amepata maumivu makubwa kiasi gani, lakini ni wazi kuwa atakuwa nje kwa wiki tatu au zaidi".