NTAMBA Band iliyo chini ya tabibu Ntamba na Mungu iko kambini ikijiandaa na ujio mpya wa kishindo, kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo, Okaroba Omega.
Hivi sasa Ntamba Band inayojumuisha vijana wanne wenye vipaji ambao ni Okaroba mwenyewe, Rayshar, AR Madini na Boker Junior inatamba na kibao chao kipya cha “Mgeni wa Nani”.
“Muda si mrefu tutaachia kazi yetu mpya ya audio pamoja na video, ambayo tunaamini itakuwa moto wa kuoteambali na itafunika vibao vyetu vyote vilivyotangulia,” ametamba Okaroba katika mazungumzo na Saluti5.