Siku ya Jumapili imeendelea kuwa ya neema kwa Jose Mourinho pale anapocheza kwenye uwanja wa nyumbani.
Kocha huyo Mreno jana aliiongoza Manchester United kuishindilia Everton 4-0 kwenye dimba la Old Trafford.
Mechi hiyo ikamfikishia Mourinho jumla ya mechi 105 za ligi kuu kwenye uwanja wa nyumbani siku za Jumapili bila kupoteza mchezo.
Mourinho ameshinda mechi 81 na sare 24 katika mechi hizo 105 za ligi kuu kwenye uwanja wa nyumbani.