Manchester City imekamata usukani wa Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua Watford 6-0 huku Sergio Aguero akifunga mara tatu.
Ili Manchester United irejee kileleni wa ligi, itahitaji kuifunga Everton 5-0 katika mchezo utakaochezwa Jumapili.
Magoli mengine ya City yalifungwa na Gabriel Jesus, Nicolás Otamendi na Raheem Sterling.
Watford (4-2-3-1): Gomes 5; Janmaat 5, Mariappa 5, Kabasele 5, Holebas 5; Chalobah 6 (Capoue 70 5.5), Doucoure 5; Carrillo 5, Cleverley 5.5 (Pereyra 65 6), Richarlison 6; Gray 6 (Deeney 74 6).
Manchester City (4-1-3-2): Ederson 7; Walker 7.5, Stones 7, Otamendi 7.5, Mendy 7.5; Fernandinho 7.5; De Bruyne 8 (Gundogan 66 6.5), D Silva 8 (Sane 78), Sterling 7.5; Aguero 8.5, Jesus 8 (B Silva 65).