Kuumia kwa Paul Pogba kunaweza kufungua mlango kwa kiungo anayesugua benchi Manchester United, Ander Herrera.
Kiungo huyo wa Kihispania ana kazi kubwa ya kumshawishi Mourinho ili kurejea kwenye kikosi chaguo la kwanza baada ya kuporwa namba na ujio wa Nemanja Matic.
Herrera, mchezaji bora wa Manchester United msimu uliopita amejikuta yuko nyuma ya Marouane Fellaini katika kipaumbele cha Mourinho msimu huu kwenye safu ya kiungo.