Cristiano Ronaldo amarejea kwa kishindo kutoka kwenye adhabu yake ya kufungiwa mechi tano baada ya kutupia wavuni magoli mawili wakati Real Madrid ikiichapa APOEL Nicosia 3-0 kwenye mchezo Ligi ya Mabingwa Jumatano usiku.
Ilimchukua Ronaldo dakika 12 kufungua akaunti ya magoli kabla hajatupia la pili kwa mkwaju wa penalti kunako dakika ya 51.
Wakati Ronaldo akifunga magoli hayo mawili, ni goli la tatu la Sergio Ramos la staili ya tikitaka ndiyo lililokuwa bao tamu zaidi.