Bendi ya Mapacha Watatu Original inayoongozwa na mwimbaji Khalid Chokoraa, kuanzia Jumamosi hii itakuwa ikipatikana katikati ya jiji la Dar es Salaam kwenye moja ya hotel kubwa za kitalii.
Chokoraa ameiambia Saluti5 kuwa bendi yake itakuwa ikipatikana Holiday Inn Hotel kila Jumamosi.
Bosi huyo wa Mapacha amesema wako katika mkataba wa majaribio ya muda mfupi na iwapo maonyesho yao yatakuwa na tija basi watapata mkataba wa muda mrefu kutumbuiza hapo Holiday Inn.
“Tutakuwa tukipiga miziki ya aina mbali mbali – ya ndani na nje ya Tanzania, tutapiga ‘copy’ za nyimbo maarufu kutoka kila pembe ya dunia,” alisema Chokoraa.