Crystal Palace inakuwa timu ya kwanza katika historia ya Premier League kufungwa mechi zote nne za mwanzo wa ligi na pia kushindwa kudumbukiza wavuni hata goli moja.
Hali hiyo pia inakiweka pabaya kibarua cha kocha Mholanzi Frank de Boer ambaye huenda akatimuliwa kabla hata ya kufika nusu ya msimu.
Crystal Palace pia inafikia rekodi ya mwaka 1924 iliyowekwa na Preston, kabla Ligi Kuu ya England haijaitwa Premier League.
Preston ilipoteza mechi nne za mwanzo na haikufunga hata bao moja, rekodi mbaya iliyodumu kwa miaka 93 kabla haijafikiwa na Crystal Palace.