Kundi la Jahazi Modern Taarab “Wana wa Nakshi Nakshi” leo usiku litarindima mjini Dodoma ndani ya ukumbi wa Perugina.
Mmoja wa wanamuziki waandamizi wa Jahazi, Ally Jay ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni maalum kwaajili mkesha wa sherehe za Muungano.
Ally ameongeza kuwa kesho siku ya Muungano Jahazi itatumbuiza Mpwapwa katika ukumbi wa Uwama Pub.