KOCHA wa Azama FC, Aristica Cioaba amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwaunga mkono katika kipindi hiki kigumu ambapo wanakabiliana na kibarua cha kusaka nafasi ya kushiriki kwenye Kombe la CAF mwakani huku wakiwa wamepoteza tumaini la kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Njia pekee ya Azam kucheza Kombe la CAF ni kutwaa ubingwa wa Kombe la FA kwani mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara zipo mikononi mwa Simba na Yanga.
Azam inatarajia kumenyana na Kagera Sugar, Toto African na Mbao huku ikitakiwa kushinda mechi hizo ili walau kujihakikishia nafasi tatu za juu.
“Tuna kikosi imara lakini ningeomba kupata sapoti kutoka kwa mashabiki kwasababu tunakabiliwa na ratiba ngumu mwezi huu,” alisema.
Azam imepoteza mwelekeo kwenye michuano ya Ligi Kuu huku njia pekee kwao ni kushinda Kombe la FA ambalo litakuwa la pili kwao baada ya kubeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.