Christian Benteke mshambuliaji wa zamani wa Liverpool aliyetemwa na kocha Jurgen Klopp, amerejea Anfield na kuwaadhibu waajiri wake wa zamani kwenye mchezo wa Premier League.
Akiichezea Crystal Palace, Benteke akafunga magoli yote mawili katika ushindi wa 2-1.
Coutinho aliitanguliza Liverpool kwa bao la dakika ya 24 lakini Benteke akasawazisha dakika ya 42 na kufunga la ushindi dakika ya 73.
Liverpool bado inabakia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi lakini iwapo Manchester United au Manchester City itashinda viporo vyake, basi Liverpool inaweza kushuka hadi nafasi ya nne au ya tano.
LIVERPOOL (4-3-3): Mignolet, Clyne (Grujic, 84), Matip, Lovren (Alexander-Arnold, 79), Milner (Moreno, 82), Lucas, Can, Wijnaldum, Coutinho, Firmino, Origi
CRYSTAL PALACE (4-2-3-1): Hennessey, Ward, Tomkins, Kelly, Schlupp, Milivojevic, Cabaye (Delaney, 82), Puncheon, Zaha (Van Aanholt, 78), Townsend, Benteke (Campbell, 88)
Goals: Benteke (42, 73)