Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes amesema mshambuliaji kinda wa klabu hiyo, Marcus Rashford ana vigezo vyote vya kufikia uwezo Cristiano Ronaldo na Neymar.
Rashford amefunga magoli 10 katika mechi 44 msimu huu na sasa Paul Scholes anaamini kinda huyu atakuwa mmoja wa washambuliaji bora duniani.
"Rashford atakuwa mshambuliaji bora, hakuna shaka juu ya hilo," Scholes aliiambia BBC Radio 5 Live. "Kasi yake ni ya maajabu. Ni mchezaji bora klabuni akiwa na umri wa miaka 19 tu.
"Tulichokiona kwake katika mchezo dhidi ya Anderlecht ni kasi ya ajabu, uwezo na mbinu za kuwapita wachezaji pinzani kama vile hawapo uwanjani".